Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais mstaafu Mwinyi afuta kauli ‘kichwa cha mwendawazimu’

Dar es Salaam.Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameamua kufuta kauli yake aliyoisema mwaka 1993, kwenye Uwanja wa Uhuru kwamba Tanzania katika soka ni kichwa cha mwendawazimu.

Rais Mwinyi alitoa kauli ya hiyo baada ya kuishudia Simba ikichapwa mabao 2-0 katika fainali ya Kombe la CAF (saa Kombe la Shirikisho Afrika) na Stella Club d'Adjamé ya Ivory Coast.

Miaka 25, baadaye Rais Mwinyi ameifuta kauli hiyo alipokuwa katika ugawaji tuzo za Simba ‘Mo Awards’, ambapo alionekana kama amefurahia tukio hilo na kuamua futa kauli yake hiyo.

 “Ndugu zangu kuanzia leo nafuta ile kauli yangu, najua mnaikumbuka kwahiyo naiondoa kabisa siku ya leo,” alisema maneno hayo kisha akaomba kuondoka ukumbini hapo baada ya kutoa tuzo ya Heshima aliyochukua Seleman Matola.

Wachezaji waliofanikiwa kuchukua tuzo Aish Manula (Kipa Bora), Erasto Nyoni (Beki bora wa mwaka), Shiza Kichuya (Kiungo Bora), Emmanuel Okwi (Mshambuliaji Bora wa Mwaka), Zainab Rashid Pazi (Mchezaji Bora wa kike), Rashid Juma ( Mchezaji Bora Chipukizi), Goli bora la mwaka (John Bocco), Masoud Djuma, Piere Lechantre, Abbas Seleman na Mohammed Habib (Tuzo ya benchi la ufundi), Saleh Kambi (Shabiki Bora), Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’ (Mhamasishaji wa mitandaoni).

Wengine ni Haji Manara (Mhamasishaji), Seleman Matola (Tuzo ya Heshima), Ubungo Terminal (Tuzo ya Tawi Bora), Salim Abdallah (Kiongozi bora wa mwaka), John Bocco (Mchezaji Bora wa Mwaka)