Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tanzania yashusha kocha Mrundi

KLABU ya Polisi Tanzania imefikia makubaliano na kocha, Joslin Sharif Bipfubusa kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao.

Joslin (37) raia wa Burundi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Malale Hamsini aliyetimkia kwa Maafande wa JKT Tanzania.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo ilizipenyezea Mwanaspoti kwamba imefikia uamuzi huo wakiamini atawasaidia kutokana na uzoefu wake.

Kocha huyu ni msaidizi wa Jimmy Ndayizeye kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burundi huku pia akifundisha klabu ya Aigle Noir ya nchini humo.