Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tanzania yaboresha kikosi

POLISI Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa wachezaji wapya waliyosajiliwa katika kikosi hicho ni kiungo wa kati Habib Kyombo aliyekuwa anaichezea NAPSA Stars FC ya Zambia, Oscar Masai (Mtibwa Sugar), Kenn Ally Mwambungu (KMC), Jafari Kabaya (Mashujaa) na Anuary Jabir (Dodoma Jiji).

BAADA ya Polisi Tanzania kupanda kucheza Ligi Kuu Bara msimu unaoanza Agosti 14, 2026, imefanya maboresho ya kikosi, ikiwaacha baadhi ya wachezaji na kuwaongeza wengine wapya wa kuongeza nguvu ya ushindani.

Miongoni mwa wachezaji wapya waliyosajiliwa katika kikosi hicho ni kiungo wa kati Habib Kyombo aliyekuwa anaichezea NAPSA Stars FC ya Zambia, Oscar Masai (Mtibwa Sugar), Kenn Ally Mwambungu (KMC), Jafari Kabaya (Mashujaa) na Anuary Jabir (Dodoma Jiji).

Chanzo cha ndani kutoka Polisi Tz kilisema: "Lazima kikosi kifanyiwe maboresho, kuna utofauti wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Championship, tunasajili wachezaji mbalimbali, pia tutabakia na baadhi watakaosaidiana na wapya."

Alipotafutwa Jabir kuzungumzia hilo amesema: "Kwangu nimezoea kutoka timu moja kwenda nyingine, hivyo sioni kama nitakuwa na changamoto kubwa sana, kikubwa najiandaa kupambana ili huduma yangu iifae Polisi Tanzania."

Kwa upande wa Masai amesema: "Ni nafasi nyingine ya kuonyesha kipaji changu, nimeaminiwa Polisi Tz natakiwa kupambana kwa bidii kuhakikisha huduma yangu inainufaisha timu."

Polisi Tanzania imerejea Ligi Kuu kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mtoano wa mwisho. Mechi ya kwanza Polisi Tanzania nyumbani ilishinda 4-0, ugenini ikafungwa 1-0.

Polisi Tanzania ilimaliza msimu uliopita wa Championship katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66, ikacheza mtoano wa kwanza ikiitandika Mbeya Kwanza kwa jumla ya mabao 7-1.

Timu hiyo imerejea Ligi Kuu baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023 ilipomaliza nafasi ya 15 ikikusanya pointi 25 zilizotokana na kucheza mechi 30, ikishinda sita, sare saba na kupoteza 17.