Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara Luvanga aanza kufunga

CLARA Pict

Muktasari:

  • Al Nassr ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake wamekita kambi nchini Hispania ikijiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa ligi na mshindano mengine.

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudia ameanza vizuri kwenye maandalizi ya msimu mpya baada ya kufunga mabao manne na asisti tatu kwenye mechgi mbili za kirafiki alizocheza.

Al Nassr ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake wamekita kambi nchini Hispania ikijiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa ligi na mshindano mengine.

Luvanga, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Al Nassr katika misimu yake mitatu iliyopita, ameanza maandalizi ya msimu kwa kasi baada ya kufunga mabao manne katika mechi mbili za kirafiki. Kiwango hicho kinaashiria mshambuliaji huyo bado anaendelea kuwa silaha muhimu kwenye safu ya mbele ya timu hiyo.

CLAR 01

Nyota huyo ameendelea kujitengenezea jina katika Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia kutokana na muendelezo wake wa kufunga mabao kwa misimu mfululizo.

Katika misimu yake mitatu akiwa Al Nassr, Luvanga amekuwa sehemu ya kikosi kinachotegemewa, akiongoza safu ya ushambuliaji na kutoa mchango mkubwa kwa timu.

Katika msimu wake wa kwanza, 2024/25 Luvanga alifunga mabao 11 na kutoa asisti saba. Msimu uliofuata alifunga mabao 21 na kutoa asisti saba.

CLAR 02

Msimu uliopita ulikuwa bora zaidi kwake baada ya kumaliza akiwa mfungaji bora, akifunga mabao 24. Rekodi hiyo imeifanya Luvanga kuendelea kutazamwa kama mmoja wa washambuliaji muhimu katika ligi hiyo, huku uwezo wake wa kutengeneza na kufunga mabao ukiwa sehemu ya nguvu yake.

CLAR 03

Wakati nyota huyo akiendelea kuonyesha ubora wake taarifa zinaeleza kuwa Luvanga ameongezewa mkataba wa miaka miwili utakaoendelea kumweka kikosini hapo hadi mwaka 2029.