Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi na rekodi mbili ZPL

Muktasari:

  •  Polisi imefanikiwa kukaa juu ya msimamo huo kwa kuifunga Uhamiaji mabao 3-1 kwenye mechi iliyochezwa Oktoba 16, 2026 katika uwanja wa Mao A, uliopo Unguja.

TIMU ya Polisi inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), imeendelea kuwa na wakati mzuri kwenye ligi hiyo baada ya kuongoza msimamo wa ligi ikiishusha JKU kileleni iliyodumu kwa masaa 24 pekee.

 Polisi imefanikiwa kukaa juu ya msimamo huo kwa kuifunga Uhamiaji mabao 3-1 kwenye mechi iliyochezwa Oktoba 16, 2026 katika uwanja wa Mao A, uliopo Unguja.

Mchezaji Salum Akida aliitanguliza bao Polisi dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kabla mapumziko, Ismail Mcha akiongeza la pili dakika ya 49 kabla Salum hajaongeza la tatu dakika 80 huku Abdul Amin akifunga bao la kufutia machozi dakika ya 85 kwa makwaju wa penalti.

Ushindi huo unaifanya Polisi kufikisha pointi 18 huku nne za mwanzo zikitofautiana kwa pointi moja jambo ambalo linaongeza presha ndani ya ligi hiyo.

JKU iliyopo nafasi ya pili ina pointi 17 ikifuatiwa na Zimamoto yenye pointi 16  nafasi tatu huku Uhamiaji ikiwa na pointi 15 nafasi ya nne.

Licha ya timu hiyo kuongoza msimamo wa ligi hiyo bado haipo salama endapo Zimamoto ikishinda mchezo dhidi ya Raskazone, Oktoba 18, 2026. Zimamoto ikishinda mchezo huo itafikisha pointi 19 hivyo itarudi tena kuongoza msimamo huo baada ya kushushwa na JKU.

Mbali na hilo, Polisi bado inaendeleza rikodi yake ya kutopeza mchezo wowote kwenye ligi hiyo katika michezo nane iliyokwishacheza.