Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Picha ya kwanza ya Ronaldinho akiwa rumande hadharani

Muktasari:

Habari mbaya zaidi kwa Ronaldinho na kaka yake ni kuwa sheria za Paraguay zinaruhusu mtu kusota rumande hata kwa miezi sita wakati upelelezi ukiendelea na hii inathibitisha ni jinsi gani ndugu hao wawili wako kwenye wakati mgumu.

ASUNCION, PARAGUAY . HURUMA! Kama utani vile gwiji wa Barcelona, Ronaldinho Gaucho anasota rumande kisa kuingia Paraguay kwa kutumia hati feki ya kusafiria akiwa pamoja na kaka yake Roberto na sasa picha ya kwanza ya staa huyo akiwa gerezani imevuja.

Ronaldinho na kaka yake walikamatwa kwa kosa la kuingia Paraguay kwa kutumia hati feki za kusafiria, pamoja na kumiliki nyaraka kadhaa feki za nchi hiyo kitu ambacho kimewaweka matatani tangu Jumamosi.

Wawili hao walipelekwa gerezani baada ya Hakimu Clara Ruiz Diaz kusaini hati ya kukamatwa kwao katika kipindi hiki ambacho kesi yao bado inaendelea, huku akidaiwa kuwaacha nje ni hatari kwa sababu wanaweza kutoroka.

Wakati watu wengi wakiwa hawaamini kama kweli Ronaldinho anasota rumande kwa kosa hilo, mwandishi wa habari maarufu wa Paraguay, Hernan Rodriguez ameweka picha ya kwanza ya staa huyo akiwa gerezani katika akaunti yake ya twitter.

Awali Ronaldinho na kaka yake Roberto waliiomba mahakama iwaruhusu kuendelea kukaa nje chini ya ulinzi wa polisi, lakini Hakimu Clara, aliamuru waende rumande bila hata kupata dhamana kwa sababu wanaweza kutoroka.

Hakimu huyo aliviambia vyombo vya habari kuwa kutokana na aina ya kesi inayowakabili wawili hao ni wazi kuwa wanaweza hata kutoroka kama wataachwa nje na ndiyo maana ameamuru wakae rumande hadi upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika.

Habari mbaya zaidi kwa Ronaldinho na kaka yake ni kuwa sheria za Paraguay zinaruhusu mtu kusota rumande hata kwa miezi sita wakati upelelezi ukiendelea na hii inathibitisha ni jinsi gani ndugu hao wawili wako kwenye wakati mgumu.

Wakati Ronaldinho na kaka yake wakiendelea kusota rumande polisi wa Paraguay wameendelea kuwakamata watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na ishu yote ya staa huyo ambayo imevuta macho ya watu wengi kutoka kila kona ya dunia.

Alhamisi wiki iliyopita wanawake wawili walikamatwa katika viunga vya Jiji la Asuncion wakihusishwa na kesi ya Ronaldinho Gaucho na kaka yake Roberto ambao bado kesi nzima imewakalia vibaya hadi sasa.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Paraguay, Federico Delfino, nyaraka ambazo zimewatia matatizoni kina Ronaldinho zilitolewa kati ya Desemba mwaka jana na Januari mwaka huu na namba zake zinamilikiwa na watu ambao bado hawajatajwa hadharani.

Lakini, wachambuzi wa mambo wanaamini wanawake hao wawili wanaweza kuwa ndiyo wamiliki halali wa hati hizo za kusafiria pamoja na nyaraka ambazo Ronaldinho na kaka yake walizitumia baada ya kuchakachuliwa.

Delfino anadai kesi inayowakabili Ronaldinho na Roberto ni kutumia nyaraka ya serikali ikiwa na maelezo ya uongo, majina kwenye nyaraka hizo yalisomeka Ronaldo de Assis Moreira (Ronaldinho) na Roberto de Assis Moreira.

Kinachesemwa hati zile ni halali, lakini hazikutolewa kwa majina hayo badala yake namba zilizopo kwenye hati hizo ni mali ya watu wengine ndiyo maana kina Ronaldinho wameingia matatani.

Wanawake wawili waliokamatwa wakihisiwa kuwa ndio wamiliki halali wa hati hizo na nyaraka zote zinazotumiwa na Ronaldinho na kaka yake ni Maria Isabel Gayoso na Esperanza Apolonia Caballero.

Wanawake hao wawili walikamatwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Jeshi la Polisi la Paraguay, huku Gaucho akiendelea kusota rumande akisubiri hatma yake ambayo inaweza kushudia akipigwa mvua.

Msala wa Ronaldinho na kaka yake ulianzia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Silvio Pettirossi, Jumatano iliyopita baada ya kuingia Paraguay wakiwa na hati za kusafiria za nchi hiyo licha ya kuwa wao si raia. Baada ya kuingia Paraguay, taarifa ilitolewa polisi ndipo walipovamiwa wakiwa hotelini na kupekuliwa kabla ya kukamatwa na sasa wako ndani.