Papaa Zahera huyu hapa...
Mapema wiki hii kamera za gazeti la Mwanaspoti lilimnasa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zaera akitoka hotelini.
Zahera ambaye alikuwa pia Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina FC anahusishwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Simba SC.
Simba SC leo mchana wametoa taarifa ya kukamilisha kutangaza benchi lao la ufundi.
Je atakuwa Zahera au mwingine? Mwanaspoti litazidi kukuhabarisha juu ya hilo usikae mbali na mitandao yetu.