Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujue mfumo mpya wa Video Sapoti, utakaozinduliwa na Kariakoo Dabi

Muktasari:

  • Mchezo huo utakwenda kuamua nani anakuwa wa kwanza kuchukua taji la ubingwa kwa msimu ujao katika mechi hiyo ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Itakapotimia saa 2:30 usiku akili ya wengi itakuwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar kutakapopigwa mchezo mkubwa wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba kuwania Ngao ya Jamii. 2026

Mchezo huo utakwenda kuamua nani anakuwa wa kwanza kuchukua taji la ubingwa kwa msimu ujao katika mechi hiyo ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwenye mchezo huo waamuzi waliopangwa ni Ahmed Arajiga ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Mohammed Mkono, Leonard Mkumbo wakati mwamuzi wa mezani akiwa Nassir Siyah.

Mchezo huo utakuwa na historia ndani yake ambapo utashuhudiwa kutumika kwa Video Sapoti ambayo itawasaidia waamuzi kuamua matukio ambayo hayakuonekana vizuri.


INATUMIKAJE

Video Sapoti ni njia nyingine yenye tofauti kidogo na Ile ya VAR ambayo imekuwa ikizoeleka zaidi lakini Shirikisho la Soka Tanzania TFF likishirikiana na Bodi ya Ligi Tanzania imeleta Video Sapoti kutokana na kutohitajika kwa gharama kubwa.

Mfumo huu ni kwamba Kila timu itapewa kadi mbili maalum ambazo zitakuwa kwenye mabenchi yao ya ambazo zitatumika kuomba kwa mwamuzi marudio ya matukio ya utata uwanjani.

Kama timu ikiona kuna kitu hakikwenda sawa basi kocha mkuu ndiye mwenye dhamana ya kwenda kwa mwamuzi akiwa na kadi kuomba tukio husika kurudiwa na mwamuzi atafanya hivyo.


HATMA YA KADI

Wakati mwamuzi akirudia tukio hilo akijiridhisha kwamba tukio husika ni kweli timu hiyo haikutendewa haki, atautangazia Uwanja mzima matokeo ya uamuzi wake kisha kuirudisha kadi hiyo kwa kocha husika.

Endapo mwamuzi akirudia tukio hilo na kugundua hakukuwa na makosa basi kadi hiyo haitatumika tena na timu husika itasalia na kadi moja pekee kwenye mechi hiyo.

Kama ikitokea timu imeomba kurudiwa kwa matukio mawili tofauti na yote yakabainika hakukuwa na makosa timu husika itakuwa imemaliza fursa hiyo kwa kadi hizo kumalizika na itaendelea na mchezo bila maombi mengine.

Inaelezwa kadi hizo zinalenga kuhakikisha muda wa mchezo haupotezwi bila sababu za msingi ambapo timu zinatakiwa kuhakikisha ziko sahihi kwenye matukio ambayo imeyaomba.


TV MAALUM, CHUMBA

kutakuwa na mtambo maalum wa kuchanganua matukio husika ambayo yote yatatokana na video za urushwaji wa matangazo, hapa Uwanja wa Amaan wamekuja raia wa kigeni sita ambao wamekuwa walipambana kufunga mitambo hiyo itakayowasaidia waamuzi kwenye chumba maalum.

Mwamuzi wa mchezo atawekewa televisheni yake pembeni kidogo ya Uwanja, atakayoitumia kujiridhisha na matukio ambayo yatakayotokea uwanjani.