Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Panda shuka ya Fufuni Ligi Kuu Zanzibar

FUFUNI Pict

Muktasari:

  • Matokeo hayo yameiacha timu hiyo katika nafasi ya 16 kwenye msimamo ikiwa na pointi tano, huku ikihitaji kuboresha kiwango na kutafuta mwendelezo wa ushindi ili kujinasua katika nafasi hiyo ya mkiani.

FUFUNI imeendelea kuwa na matokeo ya kupanda na kushuka katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), baada ya kusubiri kwa mechi 11 kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu, kabla ya kurejea kwenye mkondo wa vipigo katika mchezo uliofuata.

Timu hiyo ilivunja mwiko wa kutopata ushindi kwa kuichapa Mlandege mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja, baada ya kusota kwa dakika 990 bila kuonja ladha ya ushindi, lakini furaha hiyo haikudumu kwani katika mchezo uliofuata ilikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Zimamoto.

Matokeo hayo yanaendelea kuonesha changamoto ya Fufuni kupata mwendelezo wa matokeo mazuri, huku ikishindwa kujenga uimara wa ushindani katika michezo yake ya ligi.

Katika mchezo dhidi ya Mlandege, Fufuni ilianza ikiwa nyuma baada ya wapinzani wake kupata bao dakika ya 32 na kwenda mapumziko wakiwa mbele. Bao hilo lilizua malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa benchi la Fufuni waliodai mpira ulikuwa umetoka nje kabla ya kurudishwa uwanjani, lakini waamuzi walilikubali.

Hata hivyo, kipindi cha pili Fufuni ilibadilika na kuongeza kasi ya mashambulizi, hali iliyoifanya kusawazisha kabla ya kupata bao la ushindi na kuondoka na alama zote tatu. Kipa Abass Robert pia alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochangia matokeo hayo kwa kufanya uokoaji muhimu.

Lakini ushindi huo haukuwa mwanzo wa mabadiliko ya kudumu kama ilivyotarajiwa, kwani katika mchezo wa 12 dhidi ya Zimamoto, Fufuni ilishindwa kuendeleza kiwango hicho na kupoteza kwa mabao 2-0.

Kabla ya kuifunga Mlandege, Fufuni ilikuwa imecheza michezo 10 bila ushindi, ikikusanya sare mbili dhidi ya Raskazone (0-0) na Black Sailors (2-2), huku ikipoteza minane.

Katika vipigo hivyo, ilifungwa na Wembe bao 1-0, Polisi 2-1, KVZ 3-0, Uhamiaji 2-1, Muembe Makumbi 1-0, Chipukizi 1-0, JKU 2-0 na Kipanga 3-1.

Katika michezo yake 12 ya mwanzo, Fufuni imekusanya ushindi mmoja, sare mbili na vipigo tisa, hali inayoonesha ugumu wa safari yake katika ligi hiyo msimu huu.

Matokeo hayo yameiacha timu hiyo katika nafasi ya 16 kwenye msimamo ikiwa na pointi tano, huku ikihitaji kuboresha kiwango na kutafuta mwendelezo wa ushindi ili kujinasua katika nafasi hiyo ya mkiani.