Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege hali mbaya Zanzibar

Muktasari:

  • Alisema, timu hiyo imekuwa na kumbukumbu mbaya za kupoteza mechi huku mchezo dhidi ya Fufuni ukiweka alama ya maumivu upande wao. Fufuni iliifunga Mlandege mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mao A, mchezo uliopigwa Novemba 15, 2026.

NAHODHA Msaidizi wa Mlandege FC, Masoud Rashid Juma, amesema hawaridhishwi na mwenendo wa timu hiyo kwasasa ndio katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Alisema, timu hiyo imekuwa na kumbukumbu mbaya za kupoteza mechi huku mchezo dhidi ya Fufuni ukiweka alama ya maumivu upande wao. Fufuni iliifunga Mlandege mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mao A, mchezo uliopigwa Novemba 15, 2026.

Alisema, timu hiyo ilifunga bao la uongozi lililodumu hadi dakika ya 88 ya mchezo huo kabla ya Fufuni kusawazisha dakika 89 na kuongeza la pili dakika za nyongeza.

“Mlandege FC inaingia katika kumbukumbu isiyoridhisha baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Fufuni SC, maana tumekuwa timu ya kwanza kufungwa na Fufuni,” alisema

Masoud alisema hakuna jambo linalowaumiza katika kipindi hiki kama kupoteza michezo, akibainisha matokeo yasiyoridhisha katika michezo minne ambayo yanaitesa timu.

Alisema, wanatambua ugumu wa Ligi Kuu Zanzibar ilivyo hivyo wamejipanga kuongeza umakini na kucheza kwa tahadhari ili kuhakikisha wanarudisha heshima ya timu hiyo.

Aidha, Masoud aliwaomba radhi mashabiki wa Mlandege FC kutokana na matokeo mabaya ya michezo iliyopita, huku akiwaomba wasiache kuisapoti timu hiyo akisema uwepo wao ni chachu kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani.

Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi, Mlandege FC inashika nafasi ya 11 ikiwa na alama 11, ikifunga mabao tisa na kufungwa 14.