Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome afichua mipango ya Ufaransa

PACOME Pict


KAMA wewe ni shabiki wa Yanga ni lazima utakuwa unatamani kufahamu hali ya kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho, Pacome Zouzoua, ambaye bado anaendelea na matibabu huku akitarajia kuondoka kwenda Ufaransa kwa ajili ya mambo makubwa mawili.


Kiungo huyo aliumia mguu wa kulia kwenye mechi ya mwisho wa msimu 2025-2026 dhidi ya JKT Tanzania, kutokana na majeraha hayo uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kumuondoa kwenye usajili wa msimu wa 2026-2027.


Taarifa za ndani kutoka kwa mtu wa karibu wa kiungo huyo zililiambia Mwanaspoti, kiungo huyo ataondoka wakati wowote kwenda Ufaransa kwa sababu kuu mbili.

PACO 01

“Bado Pacome hajaondoka Bongo kwa sababu alikuwa hajatolewa chuma alichowekewa kwenye mguu, ila baada ya zoezi hilo kukamilika atakwenda Ufaransa kupewa matibabu,” amesema mtu huyo.

Ameongeza, Pacome ataingia kwenye hatua nyingine ya matibabu na itamfanya awe sawa zaidi kwani Januari 2026 sio mbali na makubaliano yanamuhitaji kurudishwa kwenye usajili dirisha dogo.

“Pacome anatakiwa kurudi kazini mwezi Januari mwakani, kwa hiyo atakwenda Ufaransa ili kupata muda zaidi wa kupata matibabu na muda mwingi wa uangalizi wa madaktari wa huko.

“Pia atakwenda Ufaransa kwa ajili ya ukaribu na familia yake, kwani ndugu zake wengi wapo kule, hivyo amehitaji muda wa kurejea nyumbani ili aweze kupata uangalizi zaidi,” amesema.

PACO 02

Mzimu wa majeraha ya kumtoa kwenye usajili Pacome ulianza kwa Yao Kouassi ambaye naye alirejea kazini msimu uliopita dirisha dogo baada ya kukaa nje msimu mzima jambo lililomfanya atolewe kwenye hesabu.

Kama Pacome angecheza msimu huu, basi angekuwa kwenye hatua za mwisho kumalizana na klabu hiyo kwani alisalia na mwaka mmoja ili mkataba wake umalizike, akiweka rekodi ya kutumika miaka mitatu mfululizo.

Muivory Coast huyo tangu atue Yanga, amekuwa miongoni mwa viungo washambuliaji wa kutegemewa, huku akifunga mabao saba msimu wa kwanza, akipachika 13 wa pili na tisa wa tatu akifikisha jumla ya mabao 29.