Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onyango: Mkinipa Inonga wameumia

BEKI kisiki wa Simba, Joash Onyango amewachambua Pascal Wawa na Henock Inonga kuwa wote ni wachezaji wazuri na kila mmoja ana mchango wake ndani ya Simba, huku akiweka wazi tofauti yao kuwa mmoja ni mwalimu uwanjani na mwingine ni mtendaji.

Watatu hao wanaunda ukuta wa Simba wakicheza beki ya kati na kila mmoja amepata nafasi ya kucheza kwenye michezo 17 ya Ligi Kuu Bara waliyocheza hadi sasa huku ikionekana Inonga na Onyango ndio waliotumika zaidi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Onyango alisema: “Nimepata nafasi ya kucheza na mabeki wote wa kati Kennedy Juma, Pascal Wawa na Inonga. Kila mmoja ana uzuri wake katika kutimiza majukumu, lakini nafikiri nikiwa na Inonga nafurahi zaidi kwa sababu tunafanya mazungumzo.

“Ukuta mzuri ni ule ambao mazungumzo yaliyopo mnaelewana ili kuweza kumrahisishia kazi Aishi Manula, tunatakiwa kuwa na mawasiliano mazuri kuanzia kwake hadi sisi tunaopambana na washambuliaji wa timu pinzani.”

Alisema wakicheza pamoja na Inonga wamekuwa wakipeana taarifa na mchezaji huyo anageuka kuwa kiongozi uwanjani, ni mwepesi wa kutoa maelekezo sio safu ya ulinzi pekee hadi wachezaji wengine amekuwa akizungumza nao.

Wawili hao kwenye michezo 17 iliyochezwa na Simba wamecheza pamoja kwenye mechi 10 kati ya 17 wakiruhusu mabao manne kati ya sita waliyofungwa.

Michezo waliyocheza pamoja ni dhidi ya Polisi Tanzania Simba ikishinda bao 1-0, Coastal Union 0-0, Yanga 0-0, KMC 1-4, Azam FC 2-1, Mbeya City 1-0, Mtibwa Sugar 0-0, Kagera Sugar 1-0, Tanzania Prisons 0-1, Mbeya Kwanza 0-1 na Biashara United 0-3.

Wakati michezo mingine saba mabeki wa kati dhidi ya Biashara United - Inonga na Wawa mzunguko wa kwanza mchezo uliisha kwa suluhu 0-0, Dodoma Jiji walicheza Wawa na Kennedy walipata ushindi wa bao 1-0, mchezo na Ruvu Shooting alicheza Onyango na Wawa waliruhusu bao moja kwenye ushindi wa mabao 3-1.

Katika mechi ya Geita Gold alipangwa Onyango na Kennedy na mchezo ulimalizika kwa ushindi wa mabao 2-1.