Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okello mdogo kuliongoza jeshi la Uganda CECAFA U-20

OKELLO Pict

Muktasari:

  • Richard anaingia kwenye mashindano akiwa na jukumu kubwa la kuliongoza jeshi la Uganda, miaka michache baada ya jina jingine la Allan Okello, kuonekana kwenye michuano kama hiyo na baadaye kusajiliwa na Yanga msimu uliopita.

JINA la Okello limeendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Uganda kwenye michuano ya CECAFA U-20, safari hii likiongozwa na Richard Okello, ambaye ameteuliwa kuwa nahodha wa kikosi cha vijana hao kitakachoshiriki mashindano hayo jijini Dar es Salaam.

Richard anaingia kwenye mashindano akiwa na jukumu kubwa la kuliongoza jeshi la Uganda, miaka michache baada ya jina jingine la Allan Okello, kuonekana kwenye michuano kama hiyo na baadaye kusajiliwa na Yanga msimu uliopita.

Allan, ambaye ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na mchango kwenye soka la Tanzania, aliwahi kuwa sehemu ya kizazi kilichoshiriki michuano ya vijana ya CECAFA mwaka 2019 kabla ya kuitumikia timu ya taifa ya wakubwa.

OKE 01

Sasa ni zamu ya Okello mdogo, Richard, kuendeleza jina hilo akiwa na jukumu kubwa zaidi ndani ya kikosi cha Uganda baada ya kupewa kitambaa cha unahodha na kocha Laryea Kingston.

Ri chard ana cheza soka la ushi ndani nchini Uganda akiwa na BUL FC, klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda, na ameingizwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 kitakachowania nafasi ya Uganda kufika fainali za CECAFA U-20. Uganda imepangwa Kundi B pamoja na Djibouti na Sudan, huku mchezo wao wa kwanza wakianza na Djibouti, Septemba 15 saa 8:00 mchana mechi itkayopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

OKE 02

Baada ya hapo, Hippos itakutana na Sudan Septemba 19 katika mchezo muhimu katika safari yao ya kusaka nafasi ya kuvuka hatua ya robo fainali. Kwa mfumo wa mashindano hayo, timu mbili zitakazofika fainali ndizo zitakazopata tiketi ya kuiwakilisha CECAFA kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20.