Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Yanga aibukia Uarabuni

ECUA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka Algeria zilidai uongozi wa JS Kabylie ulikuwa na mpango wa kumsajili moja kwa moja Ecua pindi tu mkataba wake wa mkopo utakapomalizika kwa msimu wa 2025-2026, ingawa kiwango chake hakijawaridhisha mabosi hao kukamilisha dili hilo.

WINGA wa Yanga, Celestin Ecua amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Al-Shoulla FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Saudi Arabia, baada ya kushindwa kuwika na JS Kabylie ya Algeria aliyoitumikia kwa mkopo tangu, Januari 28, 2026.

Taarifa kutoka Algeria zilidai uongozi wa JS Kabylie ulikuwa na mpango wa kumsajili moja kwa moja Ecua pindi tu mkataba wake wa mkopo utakapomalizika kwa msimu wa 2025-2026, ingawa kiwango chake hakijawaridhisha mabosi hao kukamilisha dili hilo.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga Agosti 1, 2025, akitokea Zoman FC ya Ivory Coast, alishindwa kuonyesha kiwango kizuri na kikosi hicho, jambo lililosababisha kupelekwa kwa mkopo JS Kabylie dirisha dogo la usajili la Januari 2026.

Kabla ya kujiunga na Yanga, nyota huyo alikuwa mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu wa 2024-2025, baada ya kuhusika na mabao 27, baada ya kufunga 15 na kuasisti 12 katika mechi 27 alizochezea kikosi hicho cha Zoman.

Baada ya kutua Yanga, alihusika na mabao mawili ya Ligi Kuu Bara, akifunga moja katika ushindi wa Yanga wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Oktoba 28, 2025. Pia aliasisti bao moja.

Timu nyingine alizocheza nyota huyo ni ASEC Mimosas, ES Bafing, AS Denguele na RFC Yamoussoukro zote kutoka Ivory Coast.