Nyota Njombe Mji walilia posho
Njombe. Wachezaji wa Njombe Mji wamekatishwa tamaa na kitendo cha viongozi wa timu hiyo kutowapa posho kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga.
Wakizungumza na mwandishi kambini kwao hapa Njombe, nyota hao wamesema baada ya kunyimwa posho kwenye mechi dhidi ya Yanga, hawafahamu ni lini watapewa posho tena.
Nyota mmoja raia wa Nigeria, alisema kitendo cha kutopewa chochote kimewavunja imani kabisa.
"Tuliamini kwamba mechi na Yanga ambayo ina mapato makubwa tutapewa posho lakini tumetolewa kapa, inavunja moyo sana," alisema mshambuliaji huyo.