Nyerere Cycling Toure yatoa msaada
Muktasari:
- Kupitia mpango huo, Vodacom Tanzania Foundation inasaidia upatikanaji wa madawati 1,000, ujenzi na ukarabati wa madarasa, upandaji miti na utekelezaji wa miradi mingine ya kijamii katika maeneo yanayopitiwa na msafara huo.
NYERERE Cycling Tour 2026 imeendelea kuonyesha nafasi ya mchezo wa baiskeli katika kuchochea maendeleo ya jamii, huku Vodacom Tanzania Foundation ikiunganisha msafara huo na juhudi za kuboresha elimu, kuhifadhi mazingira na kuinua ustawi wa wananchi kupitia miradi ya kijamii.
Kupitia mpango huo, Vodacom Tanzania Foundation inasaidia upatikanaji wa madawati 1,000, ujenzi na ukarabati wa madarasa, upandaji miti na utekelezaji wa miradi mingine ya kijamii katika maeneo yanayopitiwa na msafara huo.
Shule ya Msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa wanufaika wa mpango huo, ambapo taasisi hiyo imekabidhi madawati kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira yanayokidhi mahitaji yao.
Afisa Miradi ya Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation and sustainability specialist, Deborah Kaluzi, Deborah Kaluzi, alikabidhi madawati hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Yasini Shehaghilo, katika hafla iliyohudhuriwa na wadau wa elimu, wawakilishi wa Vodacom Tanzania na waendesha baiskeli.
Mchango huo unaonyesha namna mashindano ya michezo yanavyoweza kwenda zaidi ya ushindani na matokeo ya uwanjani, kwa kuwa jukwaa la kuhamasisha mshikamano, uwajibikaji wa kijamii na uwekezaji unaogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Kwa upande wa mazingira, msafara huo umetumika pia kuhamasisha utunzaji wa mazingira kupitia shughuli za upandaji miti, zinazolenga kuongeza uoto wa asili na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa, alishiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Msingi Makumbusho pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC.
Ushiriki wa waandaaji, wadau wa michezo na kampuni zinazounga mkono shughuli hizo unaimarisha nafasi ya Vodacom Nyerere Cycling Tour kama jukwaa linalounganisha michezo, utunzaji mazingira na uwajibikaji kwa jamii. Kupitia shughuli hizo, msafara huo unatoa fursa ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika juhudi za kujenga jamii bora na mazingira endelevu.