Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za Kariobangi Sharks kushushwa daraja

Muktasari:

  • Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Ligi na Mashindano ya FKF kupitia taarifa rasmi iliyosainiwa na kuwasilishwa Nairobi, Oktoba 9, 2026, baada ya kamati kupitia ripoti za waamuzi wa mchezo na maelezo kutoka kwa wahusika mbalimbali, yakiwemo mawasilisho ya viongozi wa timu hizo.

SHIRIKISHO la Soka Kenya FKF limeipa Mombasa United ushindi wa mezani wa mabao 2-0 dhidi ya Kariobangi Sharks, uamuzi ulioifanya timu hiyo ya pwani kuwa mshindi wa jumla wa mchujo na kupata nafasi ya kucheza Ligi Kuu ya Kenya, msimu wa 2026/27.

Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Ligi na Mashindano ya FKF kupitia taarifa rasmi iliyosainiwa na kuwasilishwa Nairobi, Oktoba 9, 2026, baada ya kamati kupitia ripoti za waamuzi wa mchezo na maelezo kutoka kwa wahusika mbalimbali, yakiwemo mawasilisho ya viongozi wa timu hizo.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, mchezo wa marudiano wa mchujo kati ya Kariobangi Sharks na Mombasa United ulivurugika dakika ya 64 baada ya wachezaji wa Sharks kumfuata mwamuzi wa kati wakipinga uamuzi wake wa kutoa penalti kwa Mombasa United.

Kamati ilieleza zaidi kuwa meneja wa timu ya Kariobangi Sharks, Patrick Paul Otieno, pamoja na kundi la mashabiki wa timu hiyo, waliingia uwanjani na kumshambulia mwamuzi mwilini na kumpa majeraha.


MOMBASA UNITED WAPATA TIKETI

Baada ya kutathmini ushahidi na maelezo yaliyowasilishwa, kamati iliamua kuwa Kariobangi Sharks ndiyo iliyosababisha mchezo kuvurugika na hivyo kuutangaza kuwa imepoteza kwa mujibu wa Kanuni ya 3.3.2, inayosomwa pamoja na Kanuni ya 3.3.3 ya Kanuni na Sheria zinazosimamia soka nchini Kenya za mwaka 2019.


SAKATA LA VURUGU BADO HALIJAISHA

Pamoja na uamuzi wa matokeo ya mchezo, FKF imesema masuala yanayohusiana na vurugu na utovu wa nidhamu yaliyoripotiwa wakati wa mechi hiyo yamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi kwa mujibu wa taratibu.