Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nusu fainali Dar Youth League U15 kupigwa Gymkhana

DAR Pict

Muktasari:

  • Jumla ya timu nne zimefuzu hatua hiyo ambazo ni Bulls Football Academy (Bulls FA), Simba Youth U15, West FA na Safari.

NUSU fainali ya timu za vijana wenye umri chini ya miaka 15 katika mashindano ya Dar Youth League (Dar Youth League U15) itafanyika Oktoba 3 na 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Gymkhana.

Jumla ya timu nne zimefuzu hatua hiyo ambazo ni Bulls Football Academy (Bulls FA), Simba Youth U15, West FA na Safari.

Haitakuwa vita ya kutafuta kombe pekee, bali pia jukwaa kwa vijana hao kuonyesha uwezo wao mbele ya makocha, wazazi, mashabiki na muhimu zaidi, maskauti wanaotafuta vipaji vipya.

Michezo hiyo inatarajiwa kuanza saa 8:00 mchana, huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali kutokana na kila timu kuwa na kiu ya kufika hatua ya fainali.

Dar Youth League imekuwa ikitoa nafasi kwa vijana kupata ushindani wa mara kwa mara na kujenga uzoefu unaoweza kuwasaidia kupanda hatua katika safari yao ya soka.

DA 01

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Dar Youth League, Fina Mango, amesema hatua hiyo ni matokeo ya kazi iliyofanyika kwa msimu mzima katika kuwajenga vijana.

“Hatua ya mchujo ya U15 ni kilele cha msimu uliojaa maendeleo, kujituma na kiwango kizuri kutoka kwa wachezaji wetu vijana,” amesema Mango.

Amesema lengo la mashindano hayo si kutengeneza mabingwa pekee, bali pia kuwajenga wachezaji wenye uwezo na tabia zinazohitajika ndani na nje ya uwanja.

“Tunajivunia kutoa mazingira ya ushindani yanayowasaidia vijana kukua ndani na nje ya uwanja huku tukiwahamasisha kizazi kijacho cha nyota wa soka,” amesema.

Kama kuna ushahidi mashindano hayo yanaweza kuwa daraja la kwenda kwenye soka la juu, basi Bulls FA tayari wameuonyesha.

Wachezaji watatu wa akademi hiyo wamesakwa na kuchaguliwa kujiunga na Simba Sports Club U17, hatua inayoonyesha namna vipaji vinavyoweza kuibuliwa katika mashindano ya vijana na baadaye kuingia kwenye mifumo ya klabu kubwa.

DA 02

Msimu huu pia Dar Youth League imepata sapoti kutoka kampuni ya Howden Puri, huku Mkurugenzi Mtendaji wake, Umesh Puri na wamefurahishwa kuunga mkono mpango unaotumia michezo kuwaandaa vijana.

“Howden inajivunia kushirikiana na mipango inayowapa vijana fursa na kuimarisha jamii kupitia michezo,” amesema Puri.

Amesema Dar Youth League inaendana na misingi ya maendeleo, ushirikishwaji na ubora ambayo kampuni hiyo inasimamia.

Kwa upande wa waandaaji, maskauti, klabu za Ligi Kuu, Championship na wakurugenzi wa ufundi wamealikwa kushuhudia mechi hizo kwa lengo la kuona vipaji vinavyoweza kupewa nafasi katika ngazi za juu.

Dar Youth League pia inaendesha mashindano hayo bila gharama kwa timu zinazoshiriki, ikiwa sehemu ya mpango wa kuwawezesha vijana kupata ushindani, kukuza vipaji na kujenga tabia kutokana na soka.