Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Edna Lema afafanua ishu ya kutimka Yanga Princess

EDNA Pict

Muktasari:

  • Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kocha huyo alifikia uamuzi huo muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo.

BAADA ya Yanga Princess kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026, inaelezwa kocha mkuu wa timu hiyo, Edna Lema, amejiuzulu nafasi yake, huku mwenyewe akifafanua ishu hiyo.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kocha huyo alifikia uamuzi huo muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo.

Inaelezwa Edna tayari ameshamalizana na wachezaji wa kikosi hicho pamoja na baadhi ya viongozi waliokuwa uwanjani na aliwapa mkono wa kwaheri na kuwajulisha nia yake ya kuachana nao.

ED 01

Hata hivyo, Mwanaspoti lilifanya jitihada za kumtafuta kocha huyo kwa njia ya simu ili kupata ukweli wa jambo hilo na kuzungumzia hatua hiyo inayotajwa kuishtua klabu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Edna amekanusha taarifa hizo na kuzitaja kuwa ni uvumi usio na ukweli wowote unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasioitakia mema timu hiyo.

Kocha huyo alisisitiza yeye bado ni kocha mkuu wa Yanga Princess na anaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida ndani ya klabu hiyo, huku akitaka mashabiki kupuuza taarifa hizo za kujiuzulu kwake.

ED 02

“Mimi bado ni kocha wa Yanga na nafanya kazi katika klabu hiyo, hivyo hizo ni tetesi tu za mitandaoni na hakuna kitu kama hicho,” amesema Edna Lema.

Yanga Princess ilipokea kichapo hicho kutoka kwa Simba Queens baada ya kucheza pungufu kufuatia kadi nyekundu iliyopata dakika ya 36 ya kiungo Ritticia Nabbosa.

Kipigo hicho kinaifanya Yanga Princess kupambania nafasi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Mashujaa Queens iliyopigwa bao 1-0 dhidi ya JKT Queens kwenye nusu fainali ya kwanza.