Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF yashauriwa kusimamia kanuni

ZFF Pict

Muktasari:

  • Ofisa huyo amewapongeza viongozi kushughulikia michezo nchini na kuimarisha miundombinu ya viwanja na kuwa vya kisasa.

KAMISHNA wa Jeshi la Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan, amelishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kusimamia klabu na waamuzi kudumisha nidhamu ili kuifanya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) yenye mvuto na hamasa.

Kamishna huyo, amesema endapo ZFF itasimamia sheria na kanuni kwa usawa itasaidia kuepuka migogoro isiyo ya lazima na kuipa uhai ligi hiyo. “ZFF inapaswa kuweka nguvu zaidi kwenye kusimamia klabu na waamuzi kupitia miongozo na kanuni kudumisha nidhamu kuepuka migogoro isiyo ya lazima,” amesema kamishna huyo. Sambamba na hilo, timu ya Uhamiaji imejipanga kuongeza ushindani na hamasa kwa wachezaji pamoja mashabiki ili kufika uwanjani.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa ZFF, Namala Suleiman, amesema ni vyema klabu kuimarisha vitengo vya habari kuwa wabunifu ili kuendana na mabadiliko.

Pia, Namala amesema ZFF imedhamiria kuzidisha muamko wa mashabiki kuziunga mkono timu zao na kuwaomba Uhamiaji kuweka nguvu juu ya hilo.

Ofisa huyo amewapongeza viongozi kushughulikia michezo nchini na kuimarisha miundombinu ya viwanja na kuwa vya kisasa.