Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne zampa mzuka kocha Kagera Sugar

KAZE Pict

Muktasari:

  • Tangu ajiunge na Kagera, Kaze ameiongoza timu hiyo katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara, akishinda mabao 3-1, dhidi ya Mbeya City ugenini, Oktoba 9, 2026, kisha sare nyumbani ya bao 1-1, mbele ya Polisi Tanzania, Oktoba 17, 2026.

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mrundi Cedric Kaze amesema kuiongoza timu hiyo katika mechi mbili na kupata pointi nne kati ya sita ni jambo linalovutia, huku akiwataka wachezaji wa kikosi hicho kuendelea kupambana kutokana na ushindani uliopo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaze amesema pointi nne zimempa matumaini makubwa kutokana na mwanzo mbaya wa kikosi hicho tangu alipojiunga nacho, japo kwa sasa kuna maendeleo mazuri ya mchezaji mmoja mmoja jambo linaloamsha morali kikosini.

“Bado hatujafikia kiwango tunachokihitaji lakini mechi mbili tulizopata pointi nne kwa kiasi kikubwa zimetuongezea ari ya kuzidi kupambana, Ligi ni ngumu na ili kuendana na ushindani ni lazima tujipange zaidi ya tulipo sasa,” amesema Kaze.

KAGE 02

Kaze amesema uwepo wa wachezaji wa kigeni ambao mwanzoni walikosekana kutokana na kukosa vibali vya kazi wakiwemo, beki wa kati, Boniface Onyango na kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mvuyekule kumeongeza machaguo katika nafasi hizo kikosini.

KAGE 01

Kaze aliyewahi kufundisha timu mbalimbali za Yanga, Namungo FC za Tanzania, Kaizer Chiefs FC na Sekhukhune United FC za Afrika Kusini, alijiunga rasmi na Kagera Sugar Septemba 21, 2026, akichukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Juma Kaseja.

Tangu ajiunge na Kagera, Kaze ameiongoza timu hiyo katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara, akishinda mabao 3-1, dhidi ya Mbeya City ugenini, Oktoba 9, 2026, kisha sare nyumbani ya bao 1-1, mbele ya Polisi Tanzania, Oktoba 17, 2026.