Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katwila aanza presha Geita Gold

Muktasari:

  • Taarifa za ndani ya klabu zililiambia Mwanaspoti kuwa uongozi umeamua kukutana na Katwila ili kumsikiliza na kupata ufafanuzi wa sababu zinazochangia timu hiyo kuendelea kupoteza mechi.

KOCHA Mkuu Zuberi Katwila, ameingia kwenye wakati mgumu baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Dodoma Jiji, huku mabosi wa timu hiyo wakipanga kikao cha dharura leo kutaka kujua kinachoendelea ndani ya kikosi hicho kilichoanza vizuri msimu kabla ya kupoteza mwelekeo.

Taarifa za ndani ya klabu zililiambia Mwanaspoti kuwa uongozi umeamua kukutana na Katwila ili kumsikiliza na kupata ufafanuzi wa sababu zinazochangia timu hiyo kuendelea kupoteza mechi.

Pa moja na presha kuon gezeka, mab osi hao wanataka kwanza kusikia maelezo yake kabla ya kuamua hatua zinazofuata, huku baadhi ya watu ndani ya klabu wakianza kujiuliza kama kocha huyo ana uwezo wa kurejesha makali ya kikosi.

“Kikao hicho kinatarajiwa kujikita katika tathmini ya mwenendo wa timu, maandalizi ya mechi, matumizi ya wachezaji na namna benchi la ufundi linavyoweza kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita. Lakini hakuna maamuzi yoyote ya kumfuta kazi kocha mpaka sasa.”

Katwila alikabidhiwa mikoba ya kuinoa Geita Gold Septemba 2025 kwa mkataba wa mwaka mmoja, akichukua nafasi ya Mohamed Muya baada ya timu hiyo kushindwa kupanda Ligi Kuu Bara. Hata hivyo, msimu huu wa 2026/2027, ameanza kuiongoza timu hiyo katika Ligi Kuu, ambako matarajio yalikuwa kuendeleza ushindani baada ya maandalizi na maboresho ya kikosi.

Mwanzo wa Geita Gold ulikuwa na matumaini baada ya kuichapa Mbeya City bao 1-0, kupoteza kwa Namungo bao 1-0 na kisha kuichakaza Kagera Sugar mabao 6-2. Timu hiyo pia ilitoka sare ya mabao 2-2 na Azam FC, kabla ya kufungwa na Simba mabao 2-0 na Yanga bao 1-0, matokeo yaliyoanza kuonyesha changamoto katika kuendeleza kiwango chake.Hali imezidi kuwa mbaya baada ya Geita Gold kuchapwa mabao 4-0 na Pamba Jiji, kisha kukubali kichapo kingine cha mabao 3-0 kutoka kwa Dodoma Jiji.

Geita Gold inashika nafasi ya 12 na pointi saba, itakutana na Fountain Gate  Oktoba 26.