Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma anakitu, tawimu zake za mbeba

Muktasari:

  • Ngoma raia wa DR Congo alijiunga na Yanga usajili wa dirisha kubwa lililopita akitokea Bizertin na alikuwa hajatumika kwenye mechi yoyote tangu msimu umeanza huku ikielezwa alikuwa bado hajawa fiti kuingia kwenye kikosi cha kocha mpya wa Yanga Manqoba Mngqithi ambaye amekuwa akitaka mchezaji aliye fiti asilimia 100.

BAADA ya kukosekana katika mechi nne za timu hiyo, kiungo mpya wa Yanga Freddy Ngoma juzi alianza dhidi ya Pamba Jiji na kuonyesha moto mkali kwa dakika 74 alizopewa.

Ngoma raia wa DR Congo alijiunga na Yanga usajili wa dirisha kubwa lililopita akitokea Bizertin na alikuwa hajatumika kwenye mechi yoyote tangu msimu umeanza huku ikielezwa alikuwa bado hajawa fiti kuingia kwenye kikosi cha kocha mpya wa Yanga Manqoba Mngqithi ambaye amekuwa akitaka mchezaji aliye fiti asilimia 100.

Dhidi ya Pamba ambayo Yanga ilishinda mabao 2-0, kwenye Uwanja wa KMC Complex kiungo huyo alionyesha kiwango cha juu kinachoonekana kuwakuna mashabiki wa timu hiyo ambao mara kwa mara walikuwa wakimshangilia.

Mashabiki wa Yanga walikuwa na kiu kubwa ya kumwona kiungo huyo kutokana na usajili wake kusubiriwa kwa hamu kuja kuziba nafasi iliyoachwa na Khalid Aucho ambaye tangu aondokeYanga imeonekana kupata shida eneo la kiungo mkabaji. Takwimu za mchezaji huyo zinaonyesha anaweza kuibeba timu hiyo kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu, pamoja na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo Yanga inaanza kuchanga karata zake wikiendi ijayo.

Alionekana kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye uwezo wa juu wa kupiga pasi na kipindi cha kwanza alikuwa bora zaidi baada ya kupiga pasi 62, huku kati ya hizo 61 zikifika kwa walengwa na moja ikipotea na takwimu zinaonyesha ni mmoja kati ya wachezaji waliogusa mpira mara nyingi zaidi kwa dakika hizo 45 za kwanza kipindi ambacho Yanga ilifunga mabao yake yote ya ushindi.

Kipindi cha pili kiungo huyo wa zamani pia wa AS Otôho aliendelea kuonyesha ubora na alipiga jumla ya pasi 34 huku 32 zikifika wakati mbili zilipotea, lakini jambo bora zaidi kwake ni kwamba pasi zake nyingi ni zile za kwenda mbele kama ambavyo mfumo wa Yanga wa kucheza unavyotaka.

Katika pasi hizo mbili zilizopotea, moja ilinaswa na Abdulkarim Iddy wa Pamba, tukio ambalo lilikaribia kuipa Pamba bao la kufutia machozi kama siyo hesabu kali za beki wa kati ya wa Yanga Ibrahim Abdulla ‘Bacca’ aliyeibuka na kusawazisha kwa kumdhibiti mchezaji huyo, pia alionyesha ubora wa kupokonya mipira mara nane na alitibua mashambulizi mara tatu kipindi cha kwanza, huku cha pili akifanya hivyo mara tano.

Dakika ya 74 Ngoma alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Aziz Andambwile ambaye aliwika zaidi kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba msimu uliopita na alicheza eneo hilo na kuongeza utulivu wa hali ya juu.

Hata hivyo, kocha Mngqithi aliwahi kusema, kutokuonekana kwa kiungo huyo sio ishara mbaya bali ali-hitaji muda wa kuendelea kujijenga ili awe fiti zaidi.

WASIKIE WADAU

Akizungumzia kiwango cha kiungo huyo mchezaji wa zamani Simba, Dua Said alisema mtaani kwa sasa wanasema mchezaji mpe mpira sio muda tena na hicho ndicho alichofanya Ngoma.

“Ngoma ameanza vizuri huwezi kuacha kumpongeza niliona pasi moja hivi aliipiga ilikuwa safi sana, ko-cha anayekuwa nao kambini amejua kumpanga kwa muda ule kwa sababu ana kitu cha kuisaidia timu.”

Mchambuzi wa soka Charles Abel ‘Mwandamizi’ alisema kiungo huyo mkabaji ameanza vyema ingawa maua yake yataendelea kumwagika kwa Mkenye Duke Abuya kutokana na uzoefu.

“Uwezo wake wa kupiga pasi ni mkubwa nimemuangalia nimeona anauwezo wa kusogeza timu juu.Anahitaji muda wa kumtazama huwezi kusema ubora wake moja kwa moja, bado anakazi ya kufanya.

“Kwangu ukiniwekea Duke na Ngoma namchagua Mkenya huyo ambaye anauwezo wa kuchangamsha timu anapokuwa uwanjani ukiachilia mbali uzoefu wake ndani ya ligi ya Tanzania.”