Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngassa aendeleza rekodi yake Ligi Kuu

NGASSA Pict

Muktasari:

  • Ngassa alifunga bao hilo dakika ya 17 katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Pamba Jiji, akimalizia shambulizi la kushtukiza langoni mwa wenyeji.

WINGA wa Dodoma Jiji, Benno Ngassa, ameendeleza rekodi yake ya kufunga mabao ya kwanza katika msimu wa Ligi Kuu Bara baada ya kuandika bao la kwanza msimu wa 2026/27.

Ngassa alifunga bao hilo dakika ya 17 katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Pamba Jiji, akimalizia shambulizi la kushtukiza langoni mwa wenyeji.

Bao hilo lilitokana na krosi ya William Edgar ambayo iliwakuta walinzi wa Pamba na kipa Erick Johola wakihangaika kuiondoa hatari hiyo, kabla Ngassa kujitokeza na kuumalizia mpira wavuni.

Hilo lilikuwa bao la kwanza la msimu mpya wa Ligi Kuu, huku pia likiwa bao la kwanza kwa Dodoma Jiji katika mchezo wake wa kwanza wa msimu ugenini, kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Hata hivyo, Pamba Jiji ilifanikiwa kusawazisha kupitia mshambuliaji Deogratias Mafie, na kufikia dakika ya 32 timu hizo zilikuwa zimetoka sare ya bao 1-1.

Ngassa amerudia rekodi aliyoiweka msimu uliopita, ambapo pia alikuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Dodoma Jiji bao katika msimu huo.

Katika mchezo dhidi ya Tabora United, ambayo sasa inatumia jina la TRA United, Ngassa alifunga dakika ya 52 baada ya kumalizia pasi ya mwisho kutoka kwa beki Abdi Banda.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, huku Ngassa akianza tena msimu mpya kwa kuweka jina lake kwenye rekodi ya mabao ya mapema ya Ligi Kuu Bara.