Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo yajitosa vita ya Chasambi

NAMUNGO Pict

Muktasari:

  • Chasambi aliyecheza Mtibwa Sugar na Simba, hivi karibuni alivunja mkataba wa kuitumikia Singida Black Stars, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.

NAMUNGO FC imeingia kwenye vita ya kuwania saini ya kiungo Ladack Chasambi ambaye pia anawindwa na Geita Gold, huku kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda akitajwa kuwa na nafasi kubwa katika mpango wa kumsajili mchezaji huyo.

Chasambi aliyecheza Mtibwa Sugar na Simba, hivi karibuni alivunja mkataba wa kuitumikia Singida Black Stars, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti kuwa, Namungo inataka kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji kwa kumpata winga kijana mwenye uwezo wa kucheza kwa kasi na kutengeneza nafasi, huku Chasambi akiwa miongoni mwa majina yaliyokubalika kwa Mgunda.

“Kocha anaamini Chasambi anaweza kuongeza ushindani katika kikosi chake, ndiyo maana klabu imeamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumshawishi ili kupata huduma yake, ingawa italazimika kushindana na Geita Gold ambayo nayo inahitaji saini yake,” kilisema chanzo.

Katika vita hiyo, Namungo ina faida ya kuwa na Mgunda ambaye tayari aliwahi kufanya kazi na Chasambi alipokuwa Simba, hivyo anamfahamu uwezo na aina ya mchango anaoweza kuutoa ndani ya timu.

Namungo iliyocheza mechi 11 za Ligi Kuu Bara na kukusanya pointi 15, inapambana kujiimarisha ili kukaa nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kutokana na sasa kuwa ya saba.