Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nahodha Kenya: Cecafa U-20 ni fursa

KENYA Pict

Muktasari:

  • Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kupata nafasi ya kufuzu Fainali za AFCON U-20 zitakazofanyika Ghana mwaka 2027.

NAHODHA wa timu ya Kenya U-20, Charles Junior, amesema ni hatua kubwa kwake na wenzake kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano ya CECAFA U-20, akieleza kuwa michuano hiyo ni sehemu ya kujitangaza kwao.

Junior amesema pamoja na kuingia uwanjani wakilenga kupigania ubingwa, mashindano hayo yanatoa fursa kwa vijana kujifunza, kujijenga na kuonyesha uwezo wao.

Ameongeza nafasi hiyo ya kucheza mashindano ya kimataifa ni muhimu kwa wachezaji wa umri wao kwa sababu inawapa uzoefu wa kukutana na wapinzani tofauti na kuwajenga na kuwakuza kisoka.

Hata hivyo amesema Kenya haijakwenda kwenye michuano hiyo kwa lengo la kushiriki tu, bali wanataka kutimiza malengo ya kubeba ubingwa na kufuzu kucheza Afcon.

“Lengo letu kubwa ni kubeba taji. Tunataka kufanya vizuri na kuhakikisha tunafuzu kwenda kucheza AFCON,”  amesema Junior.

KENY 02

Nahodha huyo anayekipiga Sofapaka FC ya Kenya amesema safari ya kuelekea AFCON haitakuwa rahisi kutokana na ushindani mkubwa uliopo, hivyo kila mchezaji anatakiwa kupambana, kusikiliza maelekezo ya benchi la ufundi na kucheza kwa umoja ili kufikia malengo yao.

Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kupata nafasi ya kufuzu Fainali za AFCON U-20 zitakazofanyika Ghana mwaka 2027.