Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya mabao ya Mwajanga Mbeya City

Muktasari:

  • Mwajanga ambaye msimu uliopita alikipiga Tanzania Prisons iliyoshuka daraja, kwa sasa anaitumiki Mbeya City na amekuwa bora na kuwashangaza wadau na mashabiki haswa anapotokea benchi.

WAKATI mashabiki wakiduwazwa na kiwango cha straika wa Mbeya City, Oscar Mwajanga, kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amefichua kinachoendelea baina yake na staa huyo kikosini hapo.

Mwajanga ambaye msimu uliopita alikipiga Tanzania Prisons iliyoshuka daraja, kwa sasa anaitumiki Mbeya City na amekuwa bora na kuwashangaza wadau na mashabiki haswa anapotokea benchi.

Katika mechi sita walizocheza Mbeya City, straika huyo amefunga mabao matatu na kuhusika mengine matatu na kuwa katika orodha ya vinara wa mabao kwenye Ligi Kuu akiachwa mawili na nyota wa Polisi Tanzania, Anuar Jabir mwenye matano kileleni.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayanga amesema ubora wa nyota huyo kuanzia benchi na kuingia na mabao uwanjani ni mbinu za kiufundi katika kuusoma mchezo kabla na wakati na kwamba amekuwa akimuelewa vyema.

Amesema kila kocha huwa na falsafa yake katika kumtengeneza mchezaji, hivyo anachofanya Mwajanga ni mkakati wa kumpa makali zaidi akieleza kuwa upo mfumo anautengeneza kwa wachezaji ili kufanya kweli.

“Lazima umjue mchezaji wako kutokana na mbinu za ufundi wa kocha, anachofanya Mwajanga ni kile ninachotaka japokuwa si kwake tu bali utaona wapo wachezaji wengine watatu nawatoa benchi. “Mwanjanga amekuwa na kiwango bora na kutekeleza yale ninayomuelekeza, wanaoshangaa kwamba anafunga ila anaanzia benchi wajue ni mbinu za kiufundi kwa kocha,” amesema Mayanga.

Kocha huyo ameongeza kuwa matokeo waliyonayo siyo mabaya sana japokuwa ni mapema mno kutamba kwakuwa ligi ndio inaanza kuchanganya, hivyo lazima wajipange zaidi. “Ndio maana hatujatoa muda mrefu wa kupumzika kwa vijana, kwakuwa tunajua ugumu ulivyo matokeo haya si kwamba ni mabaya ila ni mapema sana kutamba, lazima tuendelee kupambana,” amesema Mayanga.