Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwinyi Kazimoto amdunda mwandishi

Mwinyi Kazimoto.

Muktasari:

BAADA ya kiwango chake kushuka ghafla na kutokuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza cha Simba, Mwinyi Kazimoto ameanza mazoezi ya kubadili fani huku umri ukionekana kumtupa mkono.

BAADA ya kiwango chake kushuka ghafla na kutokuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza cha Simba, Mwinyi Kazimoto ameanza mazoezi ya kubadili fani huku umri ukionekana kumtupa mkono.

Kiungo huyo ambaye miaka miwili aliyoichezea Markhiya ya Qatar haikuwa na mafanikio, jana Jumatano aligeuka Tyson baada ya kumvamia na kumjeruhi kwa kipigo cha ngumi, mateke, makofi mwandishi wa gazeti hili, Mwanahiba Richard. Mwinyi anayedai kuwa na umri wa miaka 27, alifanya hivyo mjini Shinyanga.

Kazimoto aliyeonyesha wazi kuwa soka sasa limemshinda na kuutamani ubondia, alifanya hivyo mara baada ya mazoezi ya timu yake kwenye Uwanja wa Kambarage akimtuhumu Mwanahiba kumwandika vibaya katikati ya mwaka jana.

Kazimoto alimvamia Mwanahiba na kumjeruhi mwilini huku akiwa hana ushahidi wa anachokilalamikia, zaidi ya kudai aliambiwa na washikaji zake.

“Alinivamia na kunihoji kwa nini nilimwandika vibaya mwaka jana, nilimhoji ana hakika na anachokisema na kudai aliambiwa tu na washikaji zake kuonyesha anafanya mambo kwa kubahatisha,” alisema Mwanahiba akiwa hospitalini kwa ajili ya matitabu.

Mwanahiba alisema siku za nyuma Kazimoto alishawahi kumpigia simu kadhaa akimtusi na akamtisha kwa kumpa siku saba ili ataje mtu aliyempa habari aliyoiandika mwaka jana baada ya Simba kucharazwa bao 1-0 na Prisons.

“Ndipo leo (jana) baada ya mazoezi akanivamia na kunipiga, huku akitamba kuwa niende kokote na yeye hajali, hata kocha wake, Jackson Mayanja na nahodha Mussa Hassan Mgosi waliisikia, kuonyesha alikusudia,” alisema.

Mwanahiba alisema tukio hilo ameliripoti Kituo cha Polisi cha mjini Shinyanga kwa kufunguliwa jalada lenye namba SHY/RB/895/2016 kisha kupelekwa hospitali kutibiwa, huku Kazimoto akifuatwa katika kambi ya timu hiyo, iliyopo Virgimark Hotel.