Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwashiuya atambia uzoefu Bigman FC

MWASHIUYA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo iliyohamishia makazi yake jijini, Tanga zamani ikifahamika kwa jina la Mwadui FC, katika mechi 11, za msimu huu imeshinda tano, sare moja na kupoteza tano, ikiwa nafasi ya saba na pointi 16, huku ikifunga mabao 15 na kuruhusu 17.

KIUNGO mshambuliaji wa Bigman FC ya jijini, Tanga, Geofrey Mwashiuya, amesema uzoefu aliokuwa nao kwa kushirikiana na wachezaji wenzake, utakuwa ni chachu ya kukipigania kikosi hicho, ili kiweze kumaliza nafasi nne za juu kwa msimu huu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwashiuya amesema timu hiyo kwa sasa imeanza kujipata tofauti na mwanzoni na ilikuwa ni ngumu kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara katika benchi la ufundi, jambo linalowapa matumaini ya kufanya vizuri pia.

"Katika mechi tano za kwanza zilikuwa ni ngumu kwetu kwa sababu tulichelewa kuanza maandalizi ya msimu (Pre Season) kwa msimu wa 2026-2027, kisha mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi, ila kwa sasa tuko vizuri," amesema Mwashiuya.

Nyota huyo wa zamani wa Kimondo FC, Yanga, Singida United, Kagera Sugar, Mbeya City, Mbuni FC na sasa Bigman FC, amesema kwa kushirikiana na wachezaji wenzake, watapambana kumaliza nafasi nne za juu, ili wacheze mechi za mtoano 'Play-Off'.

Timu hiyo iliyohamishia makazi yake jijini, Tanga zamani ikifahamika kwa jina la Mwadui FC, katika mechi 11, za msimu huu imeshinda tano, sare moja na kupoteza tano, ikiwa nafasi ya saba na pointi 16, huku ikifunga mabao 15 na kuruhusu 17.