Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwarabu wa Man United akija patanoga

Muktasari:

Bin Salman anataka kununua hisa asilimia 91 kitu ambacho mashabiki wa Man United wanaomba kitokee ili timu hiyo iondoke kwenye mikono ya familia ya Glazer.

LONDON, ENGLAND. WANACHOWAZA mashabiki wa Manchester United itakuwaje timu yao itakapochukuliwa na mtu mwenye pesa zake, Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammad Bin Salman.

Wanaamini kitakuwa kiboko kwa Sheikh Mansour huko Manchester City katika uwekezaji kwenye timu hizo na vita yao itakuwa ya mlingano zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wanaona kama wanaburuzwa na mahasimu wao hao. Man United kwa sasa ipo chini ya umiliki wa familia ya Glazer, ambapo inadaiwa kuwa na utajiri wa Pauni 3.6 bilioni, lakini Bin Salman, peke yake anaripotiwa kuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa Pauni 7 bilioni. Ukiunganisha na utajiri wa familia yao ndio balaa zaidi. Bilionea Bin Salman, ameripotiwa kuwa na mpango wa kuinunua klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. Akitua basi itakuwa vita ya Waarabu huko Manchester.

Bosi wa Man United, Richard Arnold ameripotiwa kwenda kukutana na mabosi wa Saudi Arabia na kuamsha zaidi uvumi wa kwamba huenda mchakato wa kuiuza timu hiyo kwa Pauni 3 milioni na zaidi ukafanyika ili kumilikiwa na mwana huyo wa mfalme.

Bin Salman anataka kununua hisa asilimia 91 kitu ambacho mashabiki wa Man United wanaomba kitokee ili timu hiyo iondoke kwenye mikono ya familia ya Glazer.

Mkutano huo wa mmoja wa wajumbe wa bodi wa Man United, Arnold na mabilionea hao wa kiarabu umedaiwa kulenga zaidi katika kukamilisha mchakato wa Waraabu hao kuibeba Man United jumla. Mkutano ulifanyika nyumbani kwa Faisal Abu Saq, rafiki, ambaye huko nyuma alidaiwa kuwa na mpango wa kuinunua Man United.

Arnold alisema: “Asante kwa mapokezi haya mazuri kabisa tuliyopata hapa Riyadh. Timu yetu ina zaidi ya mashabiki bilioni moja duniani kote na mechi zetu zimekuwa zikionyeshwa na zaidi ya asilimia 80 ya vituo vya televisheni duniani. Tumekuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mashabiki 200 milioni.”

Baada ya mkutano huo, Profesa na Mwandishi wa Habari, Dr Hafez Medlej, ambaye alihudhuria tukio hilo, alisema Arnold ni kama vile alikuwa akijaribu kuthibitisha mpango wa kuiuza Man United, lakini hakuweka jambo hilo wazi kihivyo.

Mtu mwingine maarufu aliyekuwa kwenye mkutano huo ni staa wa zamani wa soka la Saudi Arabia, Sami Al-Jaber.

Mmiliki wa klabu ya Man City, Mansour anaripotiwa kuwa na utajiri wa Dola 22 bilioni hivyo watafanya vita ya utawala wa Jiji la Manchester wakati Bin Salman atakapoibeba Man United kuwa ya kibabe zaidi.