Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mganda wa TRA United asaini Geita Gold

MGANDA Pict

Muktasari:

  • Tebandeke, ambaye ana umri wa miaka 25, anajiunga na Geita Gold akitokea TRA United ambapo alikuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi msimu uliopita.

BAADA ya kurejea Ligi Kuu ya NBC, Geita Gold, imeanza kushusha majembe baada ya kufanikiwa kupata saini ya beki raia wa Uganda, Christopher Tebandeke, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Tebandeke, ambaye ana umri wa miaka 25, anajiunga na Geita Gold akitokea TRA United ambapo alikuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi msimu uliopita.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na beki huyo zinabainisha kwamba: “Tayari amemalizana na Geita Gold baada ya kufikia makubaliano mazuri kimaslahi, muda wowote atatambulishwa na timu hiyo.”

Usajili huu unamfanya Tebandeke kuitumikia timu ya pili nchini Tanzania tangu alipowasili dirisha kubwa la 2025-2026 akitokea nchini kwao Uganda, ambako alijijengea jina akiwa na klabu ya UPDF.

Kiwango chake TRA United katika msimu uliopita wa 2025-2026, beki huyu alionyesha ukomavu mkubwa akiwa na timu hiyo. Takwimu zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 21 na kuisaidia timu hiyo kumaliza kwernye nafasi nzuri katika msimu wa ligi uliopita.

Licha ya jukumu lake la kuzuia, Tebandeke alionyesha kuwa ni beki mwenye uwezo wa kufunga baada ya kufanikiwa kupachika mabao mawili. Bao lake la kwanza katika ligi ya Tanzania alilifunga Aprili 5, 2026, katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Black Stars, kisha akafunga tena Mei 20, 2026 dhidi ya Mtibwa, TRA ikishinda 2-1.

Moja ya sifa kubwa iiliyomfanya Tebandeke kutakiwa na Geita Gold ni uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ikiwemo beki wa kushoto na kati.

Kabla ya kutua Tanzania, Tebandeke alikuwa mhimili wa klabu ya UPDF nchini Uganda kwa misimu miwili (2023-2025), akicheza jumla ya mechi 36 na kusaidia timu hiyo kwa ulinzi imara.

Geita Gold, ambayo ilimaliza kuwa bingwa wa Ligi ya Championship 2025-2026 kwa alama 77, inaamini kuwa Tebandeke atakuwa kiongozi sahihi wa safu ya ulinzi.