Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yajichimbia Rwanda

AZAM Pict

Muktasari:

  • Mabosi hao kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo, wameamua kuweka kambi huko Rwanda wakiamini ndiyo hatua itakayokipa kikosi hicho makali zaidi ya kula sahani moja na Simba na Yanga kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la CRDB.

WAKATI Azam FC ikiendelea kuonyesha nguvu ya fedha kwa kusajili mastaa wa gharama kubwa kutoka ndani na nje ya Afrika, mabosi wa klabu hiyo sasa wamehamishia nguvu zao kwenye maandalizi ya msimu ujao.

Mabosi hao kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo, wameamua kuweka kambi huko Rwanda wakiamini ndiyo hatua itakayokipa kikosi hicho makali zaidi ya kula sahani moja na Simba na Yanga kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la CRDB.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabiti Zakaria, alithibitisha hilo hivyo matajiri hao wa Chamazi watakuwa timu ya tatu kutoka Ligi Kuu Bara kuweka kambi nchini humo, Simba na Singida Black Stars nazo zitakuwa huko zikishiriki michuano ya Kagame.

"Kwa sasa tunaendelea kuwatambulisha wachezaji wetu wapya na baada ya hapo tutasafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. Tunaamini kambi hiyo itatupa mazingira mazuri ya kujiandaa na ushindani unaotusubiri," amesema Thabiti.

Hatua ya kwenda Rwanda inakuja wakati Azam ikiwa tayari imewekeza bilioni  fedha katika usajili wa wachezaji watano waliotangazwa rasmi ambao kwa makadirio wameigharimu klabu hiyo zaidi ya Sh 3 bilioni bila kuhesabu gharama za mawakala, tiketi za ndege, hoteli na matumizi mengine ya usajili.

Usajili uliozua gumzo zaidi ni ule wa kiungo mshambuliaji Kipre Jr aliyerejea Chamazi akitokea MC Alger ya Algeria. Azam imelipa ada ya uhamisho ya Euro 230,000, sawa na takribani Sh 700milioni.

Katika safu ya ulinzi, Azam ilivunja benki tena kwa kumsajili beki wa kati Henri Stanic kutoka Stellenbosch ya Afrika Kusini. Beki huyo mwenye asili ya Togo na DR Congo alihusishwa na kurejea Ulaya lakini nguvu ya kifedha ya Azam ilibadili mwelekeo wake.

Chamazi pia ilifanikiwa kumng'oa kiungo mkabaji Lupini Mawuku Dieumerci kutoka Maniema Union ya DR Congo, moja ya klabu zinazojulikana kwa ugumu wa kuuza wachezaji wake. Azam ililazimika kulipa dola 400,000.

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji, Azam ilimshinda Yanga kwenye mbio za kumwania Enock Molia wa FC Lupopo. Mchezaji mwingine ni Hassan Mubiru kutoka SC Villa ya Uganda ambaye inadaiwa muda mfupi baada ya kusaini Azam, klabu moja kutoka Ulaya Mashariki ilitoa ofa ya dola 300,000.