Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muuaji Mashujaa Queens asimulia bao lake

MUUAJI Pict

Muktasari:

  • Fatma, ambaye aliingia uwanjani akiwa na jukumu la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, alitumia nafasi hiyo vizuri na kuipeleka JKT fainali kutokana na kuichapa Mashujaa Queens hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake, mechi iliyochezwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

MSHAMBULIAJI wa JKT Queens aliyesajiliwa kutoka Tanzanite Queens, Fatma Muhibu ameanza kuonyesha thamani yake kwenye kikosi hicho kipya, baada ya kufunga bao la dakika ya 48 dhidi ya Mashujaa Queens lililoipa tiketi ya fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026.

Fatma, ambaye aliingia uwanjani akiwa na jukumu la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, alitumia nafasi hiyo vizuri na kuipeleka JKT fainali kutokana na kuichapa Mashujaa Queens hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake, mechi iliyochezwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Akisimulia bao hilo, Fatma amesema hakuwa na uhakika mkubwa mwanzoni kama angeweza kufanya vizuri baada ya kupewa nafasi, lakini alijipa moyo na kuamua kutumia kile alichoelekezwa na kocha.

“Niliingia nikiwa na hofu kidogo kwa sababu haya ni mashindano yangu ya kwanza makubwa tangu nilipojiunga na JKT, lakini nilijipa moyo nikipewa nafasi niitumie vizuri,” amesema Fatma.

Amesema kabla ya bao hilo, kocha alimpa maelekezo maalumu ya kwenda upande wa kulia ambako kulikuwa na mapungufu ambayo alitakiwa kuyatumia ili kuisaidia timu.

Fatma amesema alizingatia maelekezo hayo na kuendelea kucheza kwa kujiamini, jambo lililomsaidia kufika kwenye nafasi ya kufunga na kuipatia JKT bao hilo la ushindi dakika ya 48.

“Kocha aliniambia niende upande wa kulia kwa sababu kulikuwa na nafasi. Nilipoingia nilijaribu kufuata maelekezo yake na nilipopata nafasi nikatumia vizuri,† amesema. Bao hilo lilikuwa muhimu kwa JKT Queens kwa sababu limeiwezesha timu hiyo kuondoka na ushindi dhidi ya Mashujaa Queens na kupata tiketi ya kucheza fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026 ikienda kucheza dhidi ya Simba Queens, Oktoba 3, 2026.

Kwa Fatma, zaidi ya kuisaidia timu, bao hilo limeongeza kujiamini katika mazingira yake mapya baada ya kuondoka Tanzanite Queens na kujiunga na JKT Queens, akiamini bado ana mengi ya kuonyesha iwapo ataendelea kupewa nafasi.

“Nimefurahi kwa nafasi niliyopewa na kwa kufunga bao. Kama nitaendelea kupewa nafasi, naamini bado nina mengi zaidi ya kufanya na kuisaidia timu,” amesema.