Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Queens yajipanga kutetea Ngao ya Jamii

Muktasari:

  • JKT Queens imepata ushindi huo leo Septemba 30, 2026, katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii ya Wanawake, matokeo ambayo yameipa timu hiyo tiketi ya kucheza fainali.

KOCHA wa JKT Queens, Kessy Abdallah, amesema kikosi chake kimeanza kujiandaa kwa ajili ya kutetea ubingwa wa Ngao ya Jamii Wanawake baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Queens.

JKT Queens imepata ushindi huo leo Septemba 30, 2026, katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii ya Wanawake, matokeo ambayo yameipa timu hiyo tiketi ya kucheza fainali.

Kessy amesema mchezo huo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, umewapa picha ya ushindani wanaotarajia kukutana nao msimu huu katika Ligi Kuu Soka Wanawake, huku akisisitiza kuwa dhamira yao ni kutetea taji walilolitwaa msimu uliopita.

“Mchezo wa fainali tutakuja na mpango mwingine kwamba ni lazima tutetee ubingwa wa Ngao, kwa sababu sisi ndiyo mabingwa wa msimu uliopita,” amesema Kessy.

Kessy amesema kasi na ushindani mkubwa ulioonekana katika mchezo huo umewapa tahadhari kuhusu upinzani wanaotarajia kukutana nao katika ligi msimu huu, hasa kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uzoefu wa timu za taifa.

“Kutokana na mchezo huu kuna vitu ambavyo tumeviona, kasi na ushindani ni mkubwa sana, kwa hiyo tunatarajia kukutana na upinzani mkubwa sana kwenye ligi safari hii,” amesema.

Amesema JKT Queens haikuwa na baadhi ya nyota wake kutokana na majeraha, kozi za ajira pamoja na adhabu walizopata msimu uliopita, lakini anaamini wachezaji waliopo wana uwezo wa kuendelea kuipa timu matokeo mazuri.

“Hawa tulionao ni wachezaji wetu na tunawaamini, tunawategemea. Naamini kabisa kwamba kupitia hawa watafanya vizuri,” amesema Kessy.

JKT Queens itacheza fainali Oktoba 3, 2026 dhidi ya Simba Queens kwenye Uwanja wa KMC Complex, ikiwa ni kama marudio ya msimu uliopita ambapo JKT Queens ilishinda 2-1. Simba Queens imeingia fainali kwa kuifunga Yanga Princess 3-0.