Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mukoko: Sisi tunapiga yeyote!

KIUNGO Mukoko Tonombe mchokozi sana, unaambiwa amewashusha presha mashabiki wa Yanga, huku akituma salamu kwa wapinzani wao kwenye ligi ya ndani na ile ya kimataifa akisema kile kinachoendelea kambini kwao ni maandalizi ya kuwabutua, kwani msimu huu watu watapigwa nyingi.

Akizungumza na mashabiki wa Yanga akiwa mubashara katika mtandao wake wa kijamii wa Istagram Mukoko alisema wala haoni sababu ya mashabiki wa timu hiyo kuwa wanyonge kufuatia timu yao kupoteza katika mchezo dhidi ya Zanaco.

Majibu hayo ya Mukoko yalikuja baada ya shabiki mmoja wa Yanga kumtaka raia huyo Mkongomani kutoa tathmini yake baada ya kipigo hicho kama timu yao itakuwa na uwezo kukata kiu yao ya mataji msimu ujao.

“Msiumie na matokeo ya mchezo uliopita, timu iko imara na inaendelea na mazoezi makali kambini, hakuna wasiwasi kabisa na tutarudi kwa nguvu. Ile ilikuwa ni mechi ya kirafiki tu ambayo wala hatukufanya maandalizi makubwa sana,” alisema.

Mukoko aliongeza kwamba jeuri kubwa ya Yanga kuelekea msimu ujao ni aina ya kikosi walichonacho ambapo endapo watakaa pamoja na kuzoeana tu ndani ya muda mfupi watakuwa tayari kupiga timu yoyote.

Kiungo huyo ambaye ni nahodha msaidizi aliongeza kwamba kuna ubora mkubwa wa wachezaji mmoja mmoja ambapo kila mchezaji ana kitu tofauti ambacho kitawapa thamani kubwa uwanjani msimu ujao.

“Tuna kikosi bora sana. Kitu pekee kilichobaki sasa ni wachezaji kukaa pamoja na baada ya hilo tutakuwa bora sana kuzifunga timu nyingi tutakazokutana nazo. Ukiangalia mchezaji mmoja mmoja utaona kabisa sasa tuna timu bora. Kilichobaki sasa tuwaachie makocha wakamilishe kazi yao tu na baada ya hapo mashabiki wetu mtafurahi.”


WASHAMBULIAJI MOTO

Aidha, Mukoko aliongeza kwamba safu yao ya ushambuliaji iliwasumbua sana msimu uliopita lakini msimu ujao ana imani mambo yatakuwa mazuri kwa ujio wa Heritier Makambo, Fiston Mayele na Yusuf Athuman.

Alisema washambuliaji hao wamekuwa na utofauti mkubwa wakiwa na uchu wa nyavu ambapo uzoefu wao utawaongoza kupatikana kwa mabao mengi.

“Hawa ni washambuliaji wazuri sana wanajua kutafuta mabao ukiangalia Makambo (Heritier), Fiston (Mayele) na Yusuf (Athuman) wamekuja na kitu kipya kule mbele.”



IMEANDIKWA NA LEONARD MUSIKULA