Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mugalu anawatamani Yanga

Muktasari:

STRAIKA wa Simba, Chris Mugalu amerejea rasmi mazoezini juzi Jumatatu jioni na kumwambia Mwandishi wa Mwanaspoti, Thobias Sebastian kwamba ; “Naitamani sana hiyo mechi ya Yanga.” Mugalu ambaye ni kipenzi cha mifumo ya kiuchezaji ya Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema kwa jinsi alivyopasha anajisikia yuko fiti kucheza ni suala la Kocha tu kumpa jezi.

Raia huyo wa DR Congo aliliambia Mwanaspoti kuwa anatamani sana kucheza mechi hiyo kwavile ndiyo aina ya mechi zake anazopenda.

“Nimeanza mazoezi niko vizuri, nadhani niko tayari kwa huo mchezo wa wikiendi, itategemea na maamuzi ya Kocha,”alisema mchezaji huyo mwenye nguvu za misuli.

“Napenda sana kucheza mechi kubwa na zenye ushindani kama hizi ili kujiweka kwenye rekodi za klabu na mimi vilevile kukua kisoka,”alisema Mugalu ambaye wakati fulani mashabiki wa Simba wamekuwa wakimlaumu kwa kosakosa nyingi lakini Gomes humtetea kwa sababu za kiufundi.

“Napenda sana kufunga kwenye hizi mechi kubwa,”aliongeza Mugalu ambaye ana uzoefu na soka la Afrika sasa akitamani namba ya kurudi kwenye timu yake ya Taifa ya DR Congo anakocheza Mukoko Tonombe wa Yanga.

Mechi hiyo ya watani wa jadi imeibua hisia za wengi kutokana na umuhimu wake kwa Simba katika harakati za ubingwa lakini Yanga wakipania kuchafua rekodi za Mnyama.

Yanga wamekuwa wakitamba mitandaoni kwamba sasa wanaingia na nguvu mpya ya Nabi. Yanga pia wanatambia rekodi za hivikaribuni kutopoteza dhidi ya Simba mechi ya kwanza ya mashindano wakiwa na Kocha mpya.