Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa v Geita Gold Bonge la fainali U-20

Muktasari:

  • Geita ilifuzu fainali kwa kuiondosha Kagera Sugar kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Saluja Mhoja na Frank Maganga katika mechi kali ya nusu fainali iliyopigwa juzi alasiri kabla ya jioni Mtibwa kurudia ilichokifanya msimu uliopita kwa kuing'oa Azam katika hatua kama hiyo na kwenda kubeba taji.

Dar es Salaam.Ligi Kuu ya Vijana U-20 inafikia tamati leo kwa kupigwa bonge la fainali inayozikutanisha Geita Gold na watetezi Mtibwa Sugar zilizopenya hatua hiyo baada ya kushinda mechi za mechi za nusu fainali ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Geita ilifuzu fainali kwa kuiondosha Kagera Sugar kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Saluja Mhoja na Frank Maganga katika mechi kali ya nusu fainali iliyopigwa juzi alasiri kabla ya jioni Mtibwa kurudia ilichokifanya msimu uliopita kwa kuing'oa Azam katika hatua kama hiyo na kwenda kubeba taji.

Mtibwa iliifumua Azam kwa mabao 2-1 katika mechi nyingine kali iliyopigwa jioni uwanjani hapo na kuonyesha dhamira yao ya kutaka kutetea taji kwa msimu wa tano mfululizo. Msimu uliopita timu hiyo iliifunga Azam kwa penalti 8-7 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu na kwenda kutetea taji kwa msimu wa nne mfululizo kwa kuinyoosha Mbeya Kwanza kwa mabao 4-1 kwenye fainali kali.

Katika mchezo wa juzi, Mtibwa ilipata mabao yake kupitia kwa Athuman Makambo aliyefunga dakika ya pili na kuongeza jingine kwa penalti dakika ya 15 kabla ya Azam kupata bao la kufutia machozi kipindi cha pili kupitia David Chiwalanga.

Mabao aliyofunga Makambo yamemweka kwenye nafasi nzuri ya kubeba kiatu cha Mfungaji Bora kwani alifikisha jumla ya mabao sita kwenye michuano hiyo, akimzidi aliyekuwa kinara kwenye orodha ya wafungaji wa ligi hiyo, Idd Kichindo wa Tanzania Prisons aliyekuwa na mabao matano akifuatiwa na Zidane Sereri wa Dodoma Jiji aliyefunga manne, huku timu zao zikitolewa robo fainali.

Kwa matokeo hayo ya juzi yamezifanya Mtibwa na Geita kukutana tena jioni kwenye pambano la fainali, inayosubiriwa kwa hamu kutokana na timu zote kuonyesha soka tamu tangu ligi ilipoanza Juni 21 ikishirikisha timu 16.

Kabla ya mchezo huo ambao utatoa jibu kama Mtibwa itabeba taji kwa msimu wa tano mfululizo au Geita itaandika rekodi ya kubeba taji kwa mara ya kwanza, timu za Azam na Kagera Sugar zitapepetana kwenye pambano la kusaka mshindi wa tatu, litakaloanza mapema saa 9 alasiri.