Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania Geay atwaa medali ya fedha Boston Marathon

Muktasari:

  • Hiyo ni mara ya pili Geay kushiriki mbio hizo kubwa za pesa, awali ilikuwa msimu uliopita na kumaliza wanne

Mtanzania, Gabriel Geay ametwaa medali ya fedha ya mbio za Boston marathoni ziluzomalizika jioni hii nchini Marekani.

Geay aliachwa kwa sekunde tisa na bingwa mtetezi raia wa Kenya, Evans Chebet aliyetumia saa 2:05:54.

Mtanzania huyo anayeshikilia rekodi ya taifa ya marathoni
ametumia saa 2:06:04 kumaliza mbio hiyo.

Mkenya mwingine Benson Kipruto amehitimisha tatu bora akitumia 2:06:06 huku mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kwenye marathon, Eliud Kipchoge amemaliza wa sita.