Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshikemshike wa Championship kuendelea leo

CHAMPIONSHIP Pict

Muktasari:

  • Mechi za jana Ijumaa, zilishuhudiwa vita ya maafande ikipigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya, kati ya Tanzania Prisons iliyotoka kuchapwa ugenini bao 1-0, dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiikaribisha Transit Camp iliyotoka pia kupoteza.

LIGI ya Championship imeingia raundi ya saba jana Ijumaa kwa mechi tatu kupigwa na nyingine tatu kuchezwa leo Jumamosi na kuhitimishwa kesho Jumapili, huku ushindani ukiwa ni mkali kwa timu kutafuta kujiweka katika mazingira mazuri zaidi.

Mechi za jana Ijumaa, zilishuhudiwa vita ya maafande ikipigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya, kati ya Tanzania Prisons iliyotoka kuchapwa ugenini bao 1-0, dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiikaribisha Transit Camp iliyotoka pia kupoteza.

Prisons inayoshika nafasi ya sita na pointi 10, baada ya kushinda mechi tatu, sare moja na kupoteza mbili, iliikaribisha Transit Camp iliyo nafasi ya pili na pointi 13, huku kikosi hicho kikitoka kuchapwa pia kwa mabao 2-1, mbele ya KMC FC.

CHAMP 01

Mechi nyigine za jana, KMC FC inayoongoza na pointi zake 14, ilikuwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini, Dar es Salaam kuikaribisha IAA SC ya jijini, Arusha, yenye kumbukumbu nzuri baada ya kutoka kuifunga Rhino Rangers kwa bao 1-0.

Mbeya Kwanza iliyokumbana na kichapo cha mabao 3-1, mechi iliyopita ugenini dhidi ya KenGold FC, ilikuwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kuikaribisha Kigamboni United yenye kumbukumbu ya kulazimishwa suluhu ya (0-0) na Mbuni FC.

Leo Jumamosi zitachezwa mechi tatu kali na za kuvutia, ambapo kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini, Morogoro, Songea United ambayo haijaonja ushindi hadi sasa, itaikaribisha Bandari Tanzania iliyoichapa Stand United ‘Chama la Wana’ mabao 3-0.

CHAMP 02

Katika mechi sita ilizocheza Songea United, imetoka sare tatu na kupoteza tatu, ikiwa nafasi ya 15 na pointi tatu, huku kwa upande wa Bandari ikishika nafasi ya tatu na pointi 11, baada ya kushinda tatu, ikitoka sare mbili na kupoteza moja.

Songea imekuwa na safu butu ya ushambuliaji kwani hadi sasa kikosi hicho kimefunga bao moja katika mechi sita, huku pia eneo la kujilinda likiruhusu matano, tofauti na kwa wapinzani wao Bandari Tanzania iliyofunga tisa na kuruhusu manne tu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa Songea United, Masoud Juma amesema sababu ya mwenendo wa timu hiyo ni kutokana na wachezaji kutokuwa na muunganiko mzuri wa kiuchezaji, jambo analoendelea kulifanyia kazi ili kuendana na ushindani.

CHAMP 03

“Timu inakosa balansi katika maeneo yote muhimu kwa maana ya kujilinda na lile la ushambuliaji, ni kazi ngumu kwa sababu tunahitaji kuitatua changamoto hiyo kwa haraka huku matokeo nayo pia yakiwa sio rafiki kwetu hadi sasa,” amesema Masoud.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Bandari Tanzania, Habibu Kondo, amesema timu hiyo ina mwelekeo mzuri kwa maana ya wachezaji kuanza kuelewana taratibu tofauti na mechi tatu za mwanzo, jambo linalowapa matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwa sasa.

“Mwanzo ilikuwa ngumu kwa sababu ya wachezaji wengi ni wapya na wanahitaji muda kuzoeana, nashukuru kadri wanavyocheza pamoja wanazidi kutengeneza muunganiko mzuri wa kiuchezaji na kutupa matokeo chanya kwa kiasi kikubwa,” amesema Kondo.

CHAMP 04

Kwenye Uwanja wa Samora, mkoani Iringa, wenyeji TMA FC iliyoifunga Songea United bao 1-0, itaikaribisha Gunners FC ya jijini Dodoma, huku ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kutoka kuifunga nyumbani, Bigman FC ya jijini, Tanga mabao 2-0.

Ushindi huo kwa TMA FC ulikuwa ni wa kwanza kwa kikosi hicho msimu huu, baada ya kutoka sare moja na kupoteza tatu kati ya mitano iliyocheza, ikiwa nafasi ya 13 na pointi nne, huku Gunners FC ikishika nafasi yake ya 11 na pointi zake sita.

Mechi ya mwisho leo itapigwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Morogoro, ambapo wenyeji Mtibwa Sugar iliyotoka kuichapa Tanzania Prisons bao 1-0, itaikaribisha KenGold FC ya Mbeya, yenye morali baada ya kutoka kuifunga Mbeya Kwanza mabao 3-1.

CHAMP 06

Katika mechi sita ilizocheza Mtibwa Sugar, imeshinda tatu, sare mbili na kupoteza moja, ikiwa nafasi ya tano na pointi 11, huku kwa upande wa KenGold ikishinda mbili, ikitoa sare moja na kupoteza tatu, ikishika nafasi ya 10 na pointi saba.

Raundi ya saba itahitimishwa kesho Jumapili kwa mechi mbili, ambapo Bigman FC iliyo mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi moja, itakuwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kuikaribisha Stand United iliyochapwa na Bandari Tanzania mabao 3-0.

Katika mechi sita ilizocheza Bigman FC imetoka sare moja na kupoteza tano, ikifunga mabao matano na kuruhusu 13, huku kwa upande wa Stand United inayoshika nafasi ya nane na pointi 10, ikishinda tatu, ikitoka sare moja na kupoteza moja.

CHAMP 07

Mechi ya mwisho itapigwa kwenye Uwanja wa Aga Khan, jijini, Arusha, ambapo wenyeji Mbuni FC iliyolazimishwa suluhu (0-0), dhidi ya Kigamboni United ya Dar es Salaam, itacheza dhidi ya Rhino Rangers iliyotoka kuchapwa bao 1-0 na IAA SC.

Katika mechi sita ilizocheza Mbuni FC, imeshinda moja, sare mbili na kupoteza tatu, ikiwa nafasi ya 12 na pointi tano, huku Rhino Rangers ikishika nafasi ya saba na pointi 10, baada ya kushinda tatu, sare moja na kupoteza miwili hadi sasa.