Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kondo aichorea ramani upya Bandari Tanzania

KONDO Pict

Muktasari:

  • Bandari ilimaliza vinara kundi A na pointi 32, katika Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2025-2026, baada ya kushinda mechi 10, sare mbili na kupoteza mbili kati ya 14, iliyocheza, huku ikifunga mabao 25 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa tisa.

KOCHA Mkuu wa Bandari Tanzania, Habibu Kondo amesema kiwango inachoonyesha kwa sasa timu hiyo bado hakijafikia asilimia 100 ya anayoihitaji, ingawa mwenendo wa kikosi hicho unaridhisha na unatoa picha nzuri ya kutimiza malengo waliyoyaweka.

Kocha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam FC, Coastal Union, Majimaji, Mbeya Kwanza na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 18 (U-18), amesema mwelekeo wa kikosi hicho ni mzuri sana, japo wanahitaji muda kutengeneza balansi ya kiuchezaji.

"Bado tunahitaji kucheza katika kiwango cha hali ya juu, Ligi ya Championship ni ngumu sana kwa sababu ya mahitaji ya kila mmoja wetu, mwenendo kijumla hadi sasa ni mzuri na unatupa motisha ya kuendeleza ushindani zaidi," amesema Kondo.

Kocha huyo amesema malengo ya timu hiyo ni kupanda daraja na kwenda kushiriki Ligi Kuu Bara, jambo ambalo wanaendelea kulipigania, licha ya ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wao, hususani kwa mechi za ugenini ambazo huwa ndizo ngumu.

Timu hiyo ya Mtwara, imecheza mechi sita za Championship, ikishinda tatu, sare mbili na kupoteza moja tu na safu ya ushambuliaji imefunga mabao tisa na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne, huku ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 11.

Bandari ilimaliza vinara kundi A na pointi 32, katika Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2025-2026, baada ya kushinda mechi 10, sare mbili na kupoteza mbili kati ya 14, iliyocheza, huku ikifunga mabao 25 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa tisa.