Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrithi wa Mayele Yanga huyu hapa

MASHABIKI wa Yanga huko mtaani na mitandao ya kijamii wanatamba kuwa mziki wa kusumbua msimu ujao na kama kawaida yao watabeba tena mataji, lakini kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi ametamka bado kuna staa mmoja tu, amesalia ili kufunga usajili wa klabu hiyo.

Kama hujui ni kwamba kwa sasa mabosi wa Yanga wana majina matatu mezani mwao ya mastraika ambao mmoja wao ndio atakayesajiliwa ili kuchukua nafasi ya Mayele anayjiandaa kutua Pyramids ya Misri baada ya misimu miwili ya kibabe akiwa na klabu hiyo huku akitwaa tuzo ya Mfungaji Bora.

Lakini wakati mabosi wa Yanga wakipiga hesabu ya kuchuja mchezaji gani wa kuvaa viatu vya Fiston Mayele kwa ufanisi wakati msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa ikianza mwezi ujao, kocha Gamondi ameliambia Mwanaspoti, kwa sasa anataka ashushiwe straika wa maana kuja kumalizia kazi na akataja sifa moja tu ya mtu anayemtaka vingine vyote ni mbwembwe tu kwake.

Kocha huyo raia wa Argentina alisema mabosi wake wamebakiza kumletea straika ambaye atakuja kuchukua nafasi ya Mayele na kwamba mshambuliaji atakayekuja awe na ubora mmoja tu wa kujua kufunga na sio kubahatisha.

"Tumebakiza kumleta mtu mmoja, tunahitaji kuwa na mtu wa uhakika wa kufunga pale mbele, bado tuna muda wa kumleta au kumtafuta mtu wa namna hiyo,"alisema Gamondi.

"Kwangu mimi mshambuliaji ana maanisha ubora mmoja tu muhimu, kujua kufunga, tunahitaji kuwa na mtu mwenye uhakika wa kuweka mpira wavuni na sio kitu kingine.

Gamondi aliongeza, hana budi kukubaliana kuondoka kwa Mayele aliyefanya makubwa kabla ya kocha huyo hajatua Yanga na kwamba lazima maisha yaendelee kwa kupata mrithi wake.

"Tunaheshimu sana mazuri yote aliyoyafanya Fiston (Mayele) ambaye anatarajia kuondoka, kila kocha angependa kufanya naye kazi lakini maisha lazima yaendelee kwa pande zote," alisema kocha huyo aliyeiongoza Yanga kwa mara ya kwanza juzi kwa kuifunga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.


HESABU ZILIVYO

Wakati Gamondi akisisitiza hilo Mwanaspoti linakuthibitishia mezani kwa tajiri namba moja wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed 'GSM' kuna maombi ya kupitishwa bajeti ya ujio wa mshambuliaji huyo.

Ingawa Yanga haijafanya mambo rasmi lakini Mwanaspoti linakuhakikishia rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said alikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho kumleta nchini straika Emmanuel Dikongue Mahop.

Mahop ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Cameroon msimu uliomalizika akifunga mabao 15 kwenye mechi 20, huku akitoa pasi za mabao 3.

Mshambuliaji huyo anayetumia mguu wa kushoto amewavutia mabosi wa Yanga wakipiga hesabu kumleta nchini kesho kuja kuwahi usajili wa Shirikisho Afrika CAF lililobakiza siku 7 pekee kabla ya kufungwa kuanzia leo.

Mahop kama atasajiliwa na Yanga atakuwa amewapiga bao washambuliaji wawili Sankara Karamoko wa ASEC Mimosas ambaye msimu uliopita alifunga mabao matano sawa na kiungo wake mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye Yanga imeshamchukua mapema na yupo kambini.

Mbali na majina hayo, pia mabosi wa Yanga walikuwa wakiwania saini ya mfungaji bora wa ligi ya nchini humo  Diby Bérenger anayeichezea San Pedro aliyefanikiwa kufunga jumla ya mabao 10 katika msimu uliopita.