Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri yavuja! Dalali afichua siri ya kushindwa kuifunga Yanga

DALALI Pict


KAMA kuna kitu kinachomkwaza mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ‘Field Marshal’ ni logo ya klabu hiyo kubadilishwa, bila makubaliano ya wanachama kuridhia katika mkutano mkuu, akiushauri uongozi urekebishe jambo hilo.


Amesema awali logo ilikuwa inaonyesha picha ya mnyama mwili mzima, ila kwa sasa kimesalia kichwa pekee, ambacho hakijulikani ni cha mnyama gani na kwa mtazamo wake anaona hakipendezi.


“Najiuliza aliyebadilisha hiyo logo bila kulipeleka jambo hilo katika mkutano mkuu na wanachama kuridhia ni nani! Simba ina desturi zake na makubaliano ya watu wengi ni baraka na kuna wazee waliotangulia mbele ya haki na wengine bado wapo waliliombea hilo,” amesema Field Marshal na kuongeza;

“Sijui sasa kichwa kilichobakia ni cha mnyama gani, tangu akatwe Simba kichwa timu haijachukua ubingwa, sasa kama amekatwa ina maana amekufa na mwili wake upo wapi, lazima utakuwa umeoza na ukioza unategemea kitu gani.

“Binafsi sioni kama anavutia tofauti na yule Simba mzima, ambaye alikuwa analeta uzito wa Simba akiunguruma hadi timu pinzani inaogopa alikuwa amezungushiwa kwenye duara, lakini Simba wa sasa haeleweki, niwasisitiza viongozi najua ni wasikivu wasipuuze hilo, warekebishe na logo irudiwe ya mwanzo.”

Aliyazungumza hayo wakati klabu hiyo, ikiwa inajiandaa kusherehekea miaka 90, kwamba iwe mwanzo mpya wa vitu kwenda sawa, pia akisisitiza kipindi hiki inahitajika mshikamano ili kurejesha ushindani mkali dhidi ya wapinzani wao.

“Tukiwa tunajiandaa kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwa Simba tangu mwaka 1936, basi hiyo Agosti 8, 2026 iwe na mabadiliko ya kurejesha mshikamano na umoja.”