Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morrison ampiga kijembe Manara

STAA wa Simba, Bernard Morrison amempiga kijembe
msemaji wa Yanga, Haji Manara baada ya kukomenti kwenye
posti yake huko Instagram, kwamba anapenda kwenda Uwanja
wa Ndege kuliko kubeba mataji.
Manara aliweka posti Insta, akiwahamasisha mashabiki wa
Yanga kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere kumpokea mwanamuziki wa dansi, Koffi Olomide,
ambaye atatumbuiza kwenye kilele cha Wiki ya Wananchi kesho
Jumapili uwanja wa Mkapa.


Manara aliposti tangazo lenye picha yake, akiwa ndani ya uzi
wa njano na kijani, lililokuwa na maelezo yaliyoandika
"Wananchiii...tukutane... saa sita mchana...Uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere kumpokea Mopao...Koffi Olomide"
tangazo hilo likamalizia kwa maneno ya Semaji la Wananchi
Kisha Manara akakomenti, akiandika: "Ni Emirates bro.
Airbus namba hiyo hiyo, ndio anatua nayo Mopao na mimi
nitaongoza Wananchi wenzangu kwenda Airport kumpokea Le
Koffie Charles Olomide..."
Baada ya komenti nyingi, ndipo akaunti ya Insta inayomilikiwa
na supastaa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Bernard
Morrison inayosomeka kama 'bm3gh' ilipoonekana kwenye
orodha ya waliokomenti posti hiyo ya Manara.
bm3gh aliandika hivi: "Ulikuwa unawaita 'timu ya mapokezi' na
sasa ni mtu wewe unawaongoza kwenda Airport (emoji za
kucheka) kaka mkubwa (akataja jina @hajismanara) unapenda
airport kuliko mataji (emoji ya kombe na kucheka)."
Manara amekatisha boda kutoka kuwa msemaji wa Simba hadi
kujiunga na mahasimu wa jadi wa miamba hiyo ya Msimbazi,
Yanga na kuzua gumzo kubwa kwenye soka la Tanzania na
Afrika Mashariki.