Moja Bet yawaongezea dili mashabiki wa soka

Muktasari:
Huo ni miongoni mwa michezo ya kubahatisha inayochezwa kwa njia ya mtandao.
Dar es Salaam. Mashabiki wa soka na michezo mingine wanaweza kushinda mpaka Sh milioni Moja ndani ya dakika moja kwa kutumia sh 1,000 tu kwa kucheza mchezo wa kubahatisha wa Boom Pesa uliozinduliwa jana na kampuni ya Moja Bet.
Meneja wa Hudhuma kwa wateja wa Moja Bet, Florida Mwangosi alisema wakati wa uzinduzi wa mchezo huo kuwa unachotakiwa kufanya ni kununua tiketi yenye namba kuanzia moja mpaka tisa na na kusubiri ubashiri wako ndani ya dakika hiyo moja.
Mwangosi alisema kuwa tokea kuanza kwa mchezo huo, washindi kibao wamepatikana na kuweza kuinua kipato chao kwa kutimia mchezo huo.
Alisema kuwa mchezo huo ni rahisi kucheza kwa kila mtu kwa kupitia mitandao yote ya simu cha kuzingatia ni kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 123255 na namba ya kumbukumbu 99 na kujishindia mamilioni ndani ya muda huo.
“ Huu mchezo wetu wa kubahatisha unaofahamika kwa jina la Boom Pesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea” Alisema Mwangosi .
Naye Balozi wa Boom Pesa Sabrina Ibrahimu, alisema mwitikio kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye mchezo huo wa kubahatisha ni mkubwa sana , nakwamba wananchi zaidi ya 100 kwa siku moja walijitokeza na kushiriki mchezo huo .
“ Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuupokea huu mchezo wetu mpya wa kubahatisha , nawapongeza sana maana wamekuja na baadhi wameshinda tunawashukuru sana tunawaomba waendelee kuucheza mchezo huu” Alisema Ibrahim.