Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mohamed: Najivunia tuzo ya dunia nikiwa Mwanaspoti

MWANASPOTI leo Ijumaa linaadhimisha miaka 20 tangu kuasisiwa kwake, Februari 13, 2001 na katika umri huo limepita mikononi mwa wahariri watendaji mbalimbali waliolifikisha hapa lililopo.

Miongoni mwa wahariri walioliongoza gazeti hili ni Abdul Mohamed kuanzia Februari 2014 hadi 2017 kabla ya kumpisha Ndaya Kassongo.

Abdul ameizungumzia miaka 20 ya uhai wa Mwanaspoti na kufichua anavyofarijika kuwa mmoja wa wahariri walioliongoza gazeti hili bora la michezo na burudani nchini, akisisitiza kwamba halina mpinzani Tanzania.

Mwandishi huyo mahiri wa michezo nchini, anasema gazeti hili halina mpinzani kuanzia kwa waandishi hadi mabosi wanaolisimamia kutokana na aina ya habari na uchambuzi wanaoilisha jamii.

Anasema licha ya kufanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajawahi kuona utendaji kazi uliotukuka kama wa gazeti la Mwanaspoti na kutoa ushuhuda kwamba kipindi chake alifanya zaidi ya majukumu yake na kujua waliokuwa chini yake wanahitaji nini ili kufanya kazi kwa ufasaha.

“Nimepitia vyombo vya habari vingi hapa Tanzania na Kenya, lakini Mwanaspoti lipo tofauti kabisa, habari zake zina umakini wa hali ya juu, pia unafanya kazi zaidi ya cheo, kwa maana unakuwa kama meneja wa ‘brandi’ husika, yaani stori ya mwandishi ikija uitathmini mara mbili kwa lengo la kuepuka matatizo ya kisheria,” anasema Abdul ambapo alipotoka Mwanaspoti alihamishiwa gazeti dada la Mwananchi, alikohudumu kama msanifu habari mwandamizi.

Ushauri wake kwa Mwanaspoti ni kuepuka kuandika habari za mazoea ili kushinda kasi ya mitandao ya kijamii, pia analitaka liwe suluhisho la kuwapa ukweli na uhalisia wa matukio wasomaji kwa kueleza undani na uhalisia wa matukio husika.

Juu ya jambo ambalo hatalisahau katika maisha yake ndani ya Mwanaspoti wakati akiwa mhariri mtendaji, abdul anasema: “Tukio ambalo sitalisahau wakati nipo Mwanaspoti nilipata wazo la kuandika (habari ya) uchunguzi kuhusu upangaji wa matokeo kwa kukusanya taarifa mbalimbali, niliipeleka makala hiyo kwenye tuzo za waandishi bora duniani, ya kwangu ilikuwa ya 10 kwa ubora Afrika, huo ulikuwa mwaka 2017, kwa kweli nilifarijika mno.”