Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo afunguka safari ya kuwekeza mabilioni Simba

MO DEWJI Pict

Muktasari:

  • Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti Mo ameeleza kuwa yeye ya familia yake wamekuwa karibu na Simba kwa zaidi ya miongo miwili, akisema msukumo mkubwa zaidi ni wa mapenzi na siyo wa kibiashara.

WAKATI klabu ya Simba ikiadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwake Rais wake Mohammed Dewji ameelezea kuhusu safari ya familia yake na yeye binafsi kuwekeza na kuidhamini klabu hiyo kubwa barani Afrika.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti Mo ameeleza kuwa yeye ya familia yake wamekuwa karibu na Simba kwa zaidi ya miongo miwili, akisema msukumo mkubwa zaidi ni wa mapenzi na siyo wa kibiashara.

“Unajua tangu nimezaliwa Singida baba yangu na familia yangu kwa ujumla wamekuwa wakiipenda Simba, lakini tangu nikiwa mdogo nilikuwa naipenda Simba na kuifuatilia Simba, wakati ule kulikuwa hakuna TV, tulikuwa tunaifuatilia Simba kwenye redio na baadaye nilipata uwezo mdogomdogo wa kwenda kwenye mechi zake,” amesema MO.

MO 03 (1)

Tajiri huyo kijana zaidi Afrika Mashariki na kati, amesema mahusiano kati yake na Simba yamefunguka zaidi tangu aliporudi kutoka Chuo Kikuu Marekani na mwaka 1998-99, ndipo alianza kuwa mdhamini wa Simba kwenye jezi yao walivaa MeTL na ndipo mahusiano yake na Simba yalianza kukua.

“Mimi nasukumwa zaidi na mapenzi kwa sababu ukifuatilia historia yangu tangu 1999-2001, nimekuwa karibu sana na klabu, viongozi na wachezaji wa Simba, ndiyo maana niliidhamini kwa sababu niliifanya Simba iwe na shabaha ya kuwa klabu bora Afrika,” amesema MO.

MO 05

Amesema mwaka 2001, klabu hiyo ilicheza na Zamalek ambao ndiyo walikuwa mabingwa wa Afrika na baada ya kuwaondoa katika michuano hiyo alipata funzo kutoka kwa rais wa klabu hiyo aliyemweleza mambo mengi ikiwemo ukubwa wa bajeti yao ambayo kwa wakati huo ikilinganishwa na Simba, ambayo ilikuwa ikitumia asilimia moja tu ya mabingwa hao.

“Hivyo nilirudi Tanzania na kukaa na viongozi na kuwaeleza kwamba kama tunataka kushindana na hizi timu kubwa za Barani Afrika lazima tubadili mfumo kutoka kwenye uanachama na kwenda kwenye uwekezaji na muda ule ishu ya uwekezaji ilikuwa bado haijulikani,” amesema.

MO 02

Kutokana na muundo huo kutofahamika viongozi wa Simba wa wakati ule wamesema hapana, ndipo akaamua kuwapisha, na kuamua kuingia kwenye siasa kugombea ubunge,” amesema mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Singida mjini.

Mabilioni aliyotumia Simba na mafanikio yake

Katika hatua nyingine, katika mahojiano hayo MO amesema tangu aanze kuwa mdhamini na mshirika wa klabu ya Simba yeye binafsi na MeTL wameshatumia zaidi ya Sh100 bilioni kiasi ambacho anasema ni tofauti na Sh20 bilioni za uwekezaji katika klabu hiyo.

MO 03

Aidha MO amesema kabla ya uwekezaji wake miaka minane iliyopita Simba ilikuwa haipo kwenye ramani ya soko barani Afrika hata kwenye orodha ya timu 100 bora yaani msimu wa  2016/2017 Simba haikuwepo na ilikuwea haijulikani lakini leo hii ni miongoni mwa timu bora katika bara hili.

“Leo hii tupo kwenye 10 mpaka tano bora Afrika ujue kuna kazi kubwa ambayo imefanyika kwenye hii miaka 8-10 lakini shabaha yangu tunataka kupata taji la Afrika na ili kulipata tunahitaji kufanya vitu kadhaa kujirekebisha,” amesema MO ambaye ameipa mafanikio makubwa Simba ikiwa ni pamoja na kuwa na uhakika wa kufika hatua ya robo fainali mara kwa mara kwenye michuano ya CAF, lakini pia kufanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mara moja.

MO 01

Kutokana na uwepo wa MO kwenye kikosi cha Simba, timu hiyo imekuwa ikifanya usajili mkubwa barani Afrika, lakini pia imekuwa tishio kwa kila timu kwenye bara hili.

Hata hivyo, bosi huyo amekuwa akisema mara kwa mara kuwa nia yake ni kuchukua ubingwa wa Afrika na timu hiyo jambo ambalo linaonekana kuwa linakwenda kutumia kutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa mara kwenye kikosi hicho.