Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Dewji aja na mapya Simba

MO Pict
MO Pict


BILIONEA wa Tanzania, Mohammed Dewji ambaye ni mwekezaji katika klabu ya Simba, amefunguka sababu za kutumia ukwasi wake, kampuni anayoiongoza na taasisi yake ya Mo Foundation katika klabu ya Simba huku sasa akija na mambo mapya.


Mo ambaye alikuwa akizungumza katika Mkutano wa Biashara na Benki za Biashara wa Standard Bank Group (Africa Unlocked), unaofanyika Cape Town, Afrika Kusini, amesema baada ya miaka mingi ya uzoefu, amegundua kuwa kujenga jamii kunahusu mambo mengi zaidi ya kufanya biashara akisema biashara huzalisha ustawi wa kiuchumi, uhisani hupanua fursa na michezo hujenga imani na matumaini.


“Kupitia MeTL Group, Taasisi ya Mo Dewji Foundation na uwekezaji wangu katika klabu yangu pendwa ya Simba, lengo halijawahi kuwa kujenga taasisi zenye mafanikio pekee. Lengo limekuwa kujenga taasisi zinazowaendeleza watu, kufungua uwezo wao, kukuza vipaji na kuwaandaa vijana wa kizazi kijacho ili wafikie mafanikio makubwa zaidi kuliko tuliyoyafikia sisi,” amesema.

MO Pict

Mo ambaye familia yake imekuwa ikiidhamini klabu ya Simba kwa miongo sasa, anasema mwisho wa siku, urithi wetu mkubwa hautakuwa biashara tulizozijenga, bali utakuwa watu ambao biashara hizo zimewasaidia kuwajenga.

“Sekta zinaweza kubadilika, lakini dhamira hubaki ileile. Kujenga si tukio la mara moja, bali ni mtazamo wa maisha. Ni uamuzi wa kuacha mahali, jamii au taasisi ikiwa bora zaidi kuliko ulivyoikuta,” amesema mwekezaji huyo mwenye asilimia 49 ya hisa katika klabu ya Simba.

Mo amesema kizazi kijacho kitakapokuja kututathimini kitajiuliza tulijenga nini? Je, vitatukumbuka kama kizazi kilichokuwa kikizungumzia tu uwezo wa Afrika? Au kama kizazi kilichochukua hatua na kuujenga uwezo huo kuwa uhalisia?

“Mimi tayari nina matumaini ya watakayosema. Kwamba tulichagua ujasiri badala ya starehe. Kwamba tulitengeneza thamani, si utajiri pekee. Kwamba tuliiamini Afrika kabla hata dunia haijaitambua ipasavyo. Na kwamba kwa pamoja tulijenga biashara, viwanda, taasisi na muhimu zaidi watu waliobadilisha mwelekeo wa bara letu,” amesema.

Akihitimisha hotuba yake, Mo ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu katika mkutano huo amesema enzi za kuzungumzia uwezo wa Afrika zimekwisha. Hii ndiyo enzi ya kuijenga Afrika. Hivyo basi, na tujenge kwa ujasiri. Tujenge kwa pamoja. Tujenge Afrika ambayo vizazi vijavyo vitajivunia kuirithi.

Mo pict
Mo pict

Mo Dewji alianza uwekezaji wake ndani ya Simba msimu wa 2017/2018 na kwa kipindi chake timu hiyo imefanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, pamoja na kuwa klabu tishio kwenye michuano ya CAF ikifanikiwa kufika fainali kwenye Kombe la Shirikisho na kupoteza mbele ya Berkane ya Morocco.