Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege ni kicheko tu

MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Mlandege FC imefuzu hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Urafiki FC katika mechi ya hatua ya 32 bora kwenye Uwanja wa Mao A.

KAIMU Ofisa Habari wa Mlandege FC, Ibrahim Adam Nyakunga amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kufanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la FA Kanda ya Unguja.

Mlandege FC imefuzu hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Urafiki FC katika mechi ya hatua ya 32 bora kwenye Uwanja wa Mao A.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Nyakunga amesema wachezaji walionyesha kiwango kizuri na kupambana kwa nguvu zote jambo ambalo limewapa matumaini katika mechi zijayo.

Amesema, ushindi huo ni hatua muhimu katika safari yao ya kuwania FA Cup, lakini wameweka msisitizo wa kutoridhika na mafanikio hayo, badala yake wanataka kuendelea kuongeza nguvu ili kusonga mbele zaidi katika hatua zinazofuata.

“Wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanastahili pongezi kwa kazi kubwa waliyoifanya. Walipambana na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi. Tunaamini ushindi huu utatupa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri katika hatua inayofuata,” amesema.

Amesema Mlandege FC iko tayari kukabiliana na timu yoyote itakayokutana nayo katika hatua ya 16 bora, akisisitiza malengo yao ni kwenda mbali zaidi katika michuano hiyo. Kwa upande mwingine, amewataka mashabiki na wapenzi wa Mlandege FC kuendelea kuipa sapoti timu yao kwani mshikamano kati ya wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki ni muhimu katika kuisaidia klabu kufikia malengo yake.