Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kivelege aivusha Mlandege 16 bora FA Cup

MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Mlandege ilipata ushindi huo katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Mao A, Unguja, huku Kivelege akiwa nyota wa mchezo kwa kufunga hat-trick iliyoiwezesha timu hiyo kusonga mbele.

MSHAMBULIAJI wa Mlandege FC, Boniphace Nickson Kivelege, amesema amefurahishwa na mchango wake wa kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la FA baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Urafiki SC.

Mlandege ilipata ushindi huo katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Mao A, Unguja, huku Kivelege akiwa nyota wa mchezo kwa kufunga hat-trick iliyoiwezesha timu hiyo kusonga mbele.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kivelege amesema amefurahi kutimiza moja ya malengo ya timu hiyo ya kufuzu hatua ya 16 bora, akisisitiza msimu huu wamejipanga kupambana hadi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

“Furaha yangu ni kuona tumefuzu hatua inayofuata. Tunafahamu umuhimu wa michuano hii, hivyo tutahakikisha tunafanya vizuri katika kila hatua ili kutimiza malengo yetu. Nimefurahi pia kufunga mabao matatu na kuisaidia timu kupata ushindi,” amesema.

Ameongeza, kufunga mabao ni sehemu ya majukumu yake kama mshambuliaji, hivyo anafurahi kila anapoweza kuitendea haki timu yake kwa kupata matokeo mazuri.

Hata hivyo, amesema kwa sasa wameweka pembeni furaha ya ushindi huo na kuelekeza nguvu zao katika mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Fufuni SC, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika Uwanja wa Mao A, saa 10:00 jioni.