Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwabi achukua fomu kwa njia ya mtandao

MKWABI Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa, majina ya watu wanaowania nafasi ya Mwenyekiti ambayo Mwanaspoti inayafahamu  ni Geofrey Nyange Kaburu, Anindumi Jonas na Mkwabi.

MWANASPOTI limepata taarifa kuwa Swedy Mkwabi amechukua fomu kwa njia ya mtandao kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Simba SC katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Januari 30, 2027.

Wanachama wa Simba wanaendelea na mchakato wa kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo. Fomu hizo zinatolewa katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akizungumza na Mwanaspoti, mmoja wa watu wa karibu na Mkwabi alisema kuwa mwenyekiti huyo wa zamani alichukua fomu hiyo jana jioni kwa njia ya mtandao, utaratibu unaoruhusiwa na Kamati ya Uchaguzi.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa Mkwabi hana mpango wa kufika mwenyewe katika ofisi za TFF, kwani anatarajia kumtuma mtu kuwasilisha fomu hiyo kesho, Novemba 20, 2026.

"Muda wowote atamtuma mtu kuirudisha fomu hiyo. Hataki mambo mengi wala kusindikizwa na kundi la watu. Nafikiri anapunguza kelele kwa sababu nafasi hiyo amewahi kuiongoza, hivyo hana presha kubwa. Kesho (leo) atamtuma mtu makini kuhakikisha fomu inarudishwa na kusainiwa," kilisema chanzo hicho.

Akizungumzia utaratibu wa kuchukua fomu kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, alisema:

"Kipengele cha kuchukua fomu kwa njia ya mtandao kipo. Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu linaendelea vizuri, na kila kitu kitakapokamilika tutatoa taarifa rasmi."

Mkwabi anarejea katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuiongoza Simba kwa mara ya pili, baada ya kuwahi kushika wadhifa huo kwa takribani miezi 10 kabla ya kujiuzulu, akieleza kuwa alitaka kukaa karibu na biashara zake.

Mkwabi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Simba Novemba 2018 na kujiuzulu Septemba 14, 2019.

Katika barua yake ya kujiuzulu aliyoiwasilisha kwa Bodi ya Wakurugenzi, alitaja sababu kuu kuwa ni mambo binafsi na hitaji la kupata muda zaidi wa kusimamia shughuli zake za kibiashara.

Baada ya kujiuzulu, nafasi yake ilikaimiwa kwa muda na Mwina Kaduguda kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine.

Hadi sasa, majina ya watu wanaowania nafasi ya Mwenyekiti ambayo Mwanaspoti inayafahamu  ni Geofrey Nyange Kaburu, Anindumi Jonas na Mkwabi.